Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Doto Biteko akizungumza jana kwenye mkutano wa hadhara Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na wakazi wa Wilaya ya Geita uliofanyika katika uwanja wa shule ya sekondari Bugando.
Mhe. Doto Biteko ni miongoni mwa viongozi walioambatana na Waziri
Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa kwenye ziara yake ya kikazi mkoani Geita na hapa anaeleza mafanikio katika sekta ya madini baada ya mbunge wa
Geita Vijijini Joseph Kasheku “Msukuma” kuomba maeneo ya uchimbaji kwa wajili
ya wachimbaji wadogo wa dhahabu.
Tazama Video hapa chini
Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Mhe. Joseph Kasheku "Msukuma", akiwasilisha salamu zake kwenye mkutano huo ambapo alimshukuru Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa kwa kuweka jiwe la ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Geita.
Mwenyekiti wa CCM mkoani Geita, Alhaj Said Kalidushi akiwasilisha salamu zake kwenye mkutano huo.
Mbunge wa Mbogwe, Mhe. Augustino Manyanda Masele akisalimia kwenye mkutano huo.
Mbunge wa Geita Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Costantine Kanyasu akisalimia kwenye mkutano huo.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Geita. Ni baada ya Kituo cha Afya Nzera kupandishwa hadi kuwa hospitali ya wilaya hiyo.
Serikali imetenga shilingi Bilioni 1.5 kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Geita Nzera ambapo shughuli hiyo imepangwa kukamilika ifikapo mwezi April mwakani.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na wakazi wa Geita (hawako kwenye picha) kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa shule ya sekondari Budando.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (kushoto), akisalimiana na Naibu Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko.
Sehemu ya wakazi wa Geita waliojitokeza kwa wingi kumsikiliza Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa shule ya sekondari Bugando.
Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo, BMG
No comments:
Post a Comment