Waziri wa Madini Angellah Kairuki (kushoto) na Mkuu wa MKoa wa Ruvuma Christina Mdeme (kulia ) wakichanganya kokoto katika Kituo ch Umahiri Songea wakati wa ziara Kairuki kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho
Waziri wa Madini Angellah Kairuki kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mdeme (katikati) na Mkuu wa Wilaya ya Songea Ploliti Mgema wakijadiliana jambo wakati Waziri Kairuki alipomtembelea Mkuu huyo wa Mkoa ofisini kwake.
Baadhi ya Mafundi wakiendelea na ujenzi wa Kituo cha Umahiri Songea.
Na Asteria Muhozya, Songea
Serikali
imesema haijaruhusu uchimbaji wa Madini katika Mto Muhuwesi na kwamba tayari Wizara
ya Madini ilikwishakutoa maelekezo yapatayo matano ambayo wahusika wanatakiwa kuyafanyia
kazi ili itoe maamuzi.
Hayo
yalielezwa na Waziri wa Madini Angellah
Kairuki wakati wa ziara yake ya kukagua
maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Umahiri Songea, wakati akitoa ufafanuzi kwa
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme
ambaye alimwomba Waziri asimamishe
uchimbaji huo na kwamba tayari Mkoa umezuia shughuli hizo kuendelea kwa kuwa ndiyo chanzo cha maji mkoani humo na kwamba,
alifanya hivyo ili kulinda miundombinu ya barabara.
Waziri
Kairuki alimweleza Mkuu wa Mkoa huyo kuwa, wizara ilitoa maelekezo kwa wahusika kwamba wanatakiwa kuwasilisha barua ya ridhaa ya Waziri wa
Maji, ridhaa ya Wakala wa Barabara nchini (TANROAD), ridhaa ya Bodi ya Bonde la
Mto Ruvuma/Pwani na Kusini ili wizara ijiridhishe kabla ya kutoa maamuzi.
“
Tunataka tujiridhishe na approval
kutoka katika maeneo hayo na vikipatikana vyote, nitafanya uamuzi. Kwa sasa ipo
ridhaa ya bodi ya bonde la mto Ruvuma,” alisisitiza Waziri Kairuki
Pia,
akifafanua kuhusu kusimama kwa shughuli
za uchimbaji wa madini ya Uranium unaofanywa na Kampuni ya Mantra Tanzania Limited, waziri Kairuki alisema kuwa, kampuni hiyo iliomba kusisitisha shughuli zake
kwa kipindi cha miaka mitano kutokana na
bei ya madini hayo kushuka katika soko la dunia na kwamba , suala hilo bado
linafanyiwa kazi kitaalam na kiuchumi hivyo, bado serikali haijatoa majibu
kuhusu suala husika.
Kuhusu upatikanaji wa masoko kwa wachimbaji wa
madini, Waziri Kairuki alieleza kuwa, tayari
serikali imepanga kuanzisha masoko ya madini katika maeneo mbalimbali nchini, na hivyo kutoa rai kwa Wakuu wa Mikoa nchini kutenga maeneo kwa ajili
ya uanzishwaji wa masoko hayo. Waziri Kairuki
alitoa ufafanuzi kwa Mkuu wa Mkoa
wa Ruvuma Christina ambaye alitaka kujua ni namna gani serikali inawasaidia
wachimbaji wadogo kupata masoko ya kuuzia madini madini yao.
“Mhe.
Waziri Mkoa wetu umejaliwa kuwa na madini ya aina mbalimbali na madini haya
yamekuwa ni kichocheo cha uchumi. Sasa, bado wachimbaji wetu wanapata
changamoto ya masoko kwa ajili ya kuuza madini yao,” alisema Mkuu wa Mkoa
Mndeme.
Akizungumzia
ujenzi wa Vituo vya Umahiri, Waziri
Kairuki alisema, ujenzi wa vituo vya umahiri vinavyojengwa maeneo mbalimbali
nchini vinagharimu takribani Bilioni 11
ambao ni mkopo kutoka Benki ya Dunia. Aliongeza kuwa, Songea
ni eneo ambalo serikali inaliangalia kwa
ajili ya kuanzisha shughuli za ukataji
na uongezaji thamani madini.
Alisema
kuwa, serikali iliona umuhimu wa kuwepo na vituo hivyo kutokana na
wananchi wengi kutamani kuingia katika
shughuli za uchimbaji lakini bado uchimbaji wao umekuwa si salama na wenye tija
hivyo, uwepo wa kituo hicho utawezesha kutoa elimu ya uchimbaji sahihi na wenye
tija.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Christina Mndeme akizungumzia uwepo wa kituo hicho
alisema, kukamilika kwa kituo hicho kutawezesha shughuli za uongezaji thamani
madini kufanyika mkoani humo, kupanua wigo wa shughuli za uchimbaji na
wachimbaji kuchimba kwa faida.
Aliongeza
kwamba, wachimbaji watapata taarifa sahihi wa mahali gani wauze madini yao na pia uwepo wake utawezesha kutangaza aina ya madini
yanayopatikana mkoani huo.
Vilevile,
alisema kuwa, kituo hicho kitawezesha kupunguza migogoro kati ya wachimbaji
wadogo na wakubwa kwani kitawezesha kupata taarifa sahihi za wapi wachimbe
madini.
Naye,
Afisa Madini Mkoa wa Ruvuma Abraham Nkya alisema kuwa, ujenzi wa kituo hicho
utawezesha kurahisisha upatikanaji wa takwimu za madini za mkoa huo, wachimbaji
kupata elimu ya utaalamu wa uchenjuaji bora wa madini, elimu ya ujasiliamali wa
shughuli za madini, afya na usalama mahali pa kazi.
Pia,
aliongeza kuwa, uwepo wa kituo hicho chenye nafasi kubwa, kitaweza kuwahudumia
wachimbaji wengi zaidi.
Waziri
Kairuki alitembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Songea Novemba 26.
No comments:
Post a Comment