Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus E. Mwangela akikagua shughuli za wachimbaji wadogo wa madini Wilayani Songwe ambapo ameagiza Ofisi ya Madini kuwatembelea wachimbaji na kuwapa elimu kuhusu sheria na taratibu za uchimbaji wa madini.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen.
Nicodemus E. Mwangela akiwa na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa
wamesuluhisha mgogoro baina ya wakazi wawili wa kijiji cha Saza Wilaya ya
Songwe kuhusu eneo la uchimbaji wa madini.
Brig. Jen. Mwangela amesema Suzan
Karan amebainika kisheria kuwa ni mmiliki halali wa eneo lililokuwa likigombewa
kwa kuwa ana leseni halali huku Elimbotwa Naftari ambaye hana leseni na amekuwa
akidai umiliki wa eneo hilo amebainika kuendesha shughuli za uchimbali kinyume
na sheria.
“Sheria inamtambua Suzan kama mmliki
halaki kwakuwa anayo leseni na amefuata taratibu na sheria za uchimbaji madini,
tunashauri Elimbotwa kama atataka kuendelea kuchimba madini katika eneo hilo
basi akubaliane na Suzan kufanya naye kazi”, amesisitiza.
Ameongeza kuwa serikali za vijiji
hazina mamlaka ya kuwapa vibali vya uchimbaji wawekezaji wa madini bali leseni
na vibali vyote vya uchimbaji wa madini hutolewa na ofisi za madini Wilaya,
mkoa au kanda, hii inatokana na kuwa serikali ya kijiji ilimtambua Elimbotwa
kama mmiliki wa eneo la uchimbaji kinyume na sheria.
Kwa upande wake Elimbotwa amesema
anamtambua Suzan kama mmliki halali wa eneo walilokuwa wakiligombania isipokuwa
sasa anadai fidia ya zaidi ya shilingi milioni 190 ikiwa ni gharama ya vitu
alivyowekeza kabla ya Suzan kupewa leseni ya eneo hilo.
Naye Suzan ameupongeza uongozi wa
Mkoa kwa kutoa suluhu ya mgogoro huo kutokana na kuwa ulipelekea kusimama kwa
shughuli za uchimbaji na hivyo kuathiri uchumi wake.
Aidha Brig. Jen. Mwangela ameagiza
Takukuru, TRA na taasisi zinazoweza kufanya ukaguzi, zihakiki madai ya
Elimbotwa kama ni halisi ili Suzan aweze kuyalipa.
Imeelezwa kuwa baadhi ya
migogoro ya haki ya kumiliki maeneo ya uchimbaji wa madini mkoani Songwe
inasababishwa na ukiukwaji wa taratibu na sheria za madini unaofanywa na baadhi
ya watendaji na wachimbaji.
No comments:
Post a Comment