Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo, Ruvuma
Naibu Katibu Mkuu Wa wizara ya kilimo Prof Siza Tumbo amefanya ziara ya kikazi katika mkoa wa Ruvuma ambapo pamoja na mambo mengine amehakiki usimamizi wa maghala ambao kwa sasa unasimamiwa na Bodi ya usimamizi wa stakabadhi ya ghala na Usimamizi wa ziada wa Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Bodi ya Nafaka na Mazao mchanganyiko.
Prof amehakiki taarifa za Ubora wa maghala kama zilivyopitishwa na Bodi ya usimamizi wa Stakabadhi ya ghala (Warehouse Receipt Regulatory Board-WRRB) pamoja na Ubora wa ghala sambamba na kuhakiki uwezo wa maghala na kiasi kilichopo ghalani, na kuhakikisha taarifa ya umiliki wa Korosho zilizopo kwenye ghala.
Akizungumza na wananchi wanaofanya kazi ya kubangua korosho katika kiwanda cha Korosho cha ETG kilichopo mjini Tunduru Mkoani Ruvuma Prof Tumbo amewatoa wasiwasi kuwa serikali imejidhatiti kusimamia kwa weledi Maendeleo ya wananchi kupitia viwanda.
Alisema kuwa Kiwanda hakitafungwa kwani Serikali inafanya mipango ya kuhakikisha mali ghafi inapatikana ili waweze kuendelea na kazi.
Aidha, amehakiki kiasi cha Korosho kwenye ghala kwa kupitia nyaraka za mapokezi ya Korosho kwenye ghala ambazo zinawasilishwa na Vyama vya msingi (AMCOS) na kuoanisha taarifa hizo na taarifa zilizomo kwenye taarifa za stakabadhi ya ghala (Warehouse Report).
MWISHO.
No comments:
Post a Comment