Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akiongoza kikao kazi cha wataalamu mbalimbali wanaoshughulikia Opareshini ya ununuzi wa Korosho katika Mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma kilichofanyika katika Ukumbi wa Bodi ya Korosho (CBT) kujadili mwenendo wa ununuzi wa zao hilo Leo tarehe 28 Novemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo wakati akiongoza kikao kazi cha wataalamu mbalimbali wanaoshughulikia Opareshini ya ununuzi wa Korosho katika Mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma kilichofanyika katika Ukumbi wa Bodi ya Korosho (CBT) kujadili mwenendo wa ununuzi wa zao hilo Leo tarehe 28 Novemba 2018.
Kikao kikiendelea
Na Mathias Canal-Wizara ya
Kilimo, Mtwara
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet
Hasunga Leo tarehe 28 Novemba 2018 amezuru Mkoani Mtwara kwa ajili ya ziara ya
kikazi.
Katika ziara hiyo Mhe
Hasunga atafatilia mwenendo wa ununuzi wa Korosho za wakulima katika
kuhakikisha maelekezo ya serikali yanatekelezwa.
Mara baada ya kuwasili
Mkoani humo Mhe Hasunga amekutana na wataalamu mbalimbali wanaoshughulikia
Opareshini ya ununuzi wa Korosho katika Mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma na
kufanya kikao kizito kilichofanyika katika Ukumbi wa Bodi ya Korosho (CBT)
kujadili mwenendo wa ununuzi wa zao hilo.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment