Na George Binagi-GB Pazzo
Waziri Mkuu
wa Tanzania, Kassim Majaliwa, Novemba 30, 2018 amehitimisha ziara yake ya siku
nne mkoani Geita kwa kuzungumza na wakazi wa Katoro akiwa njiani kuelekea
uwanja wa ndege Chato ambapo pamoja na mambo mengine alikasirishwa kusikia
wafanyabiashara wamechangishwa fedha kwa ajili ya mafuta ya ukarabati wa
barabara za mitaa.
Majaliwa
alisisitiza kwamba serikali haitawavumilia baadhi ya watumishi wasio waadilifu
ambao wanatafuna fedha za maendeleo ambapo akiwa katika wilaya ya Nyang’hwale
aliagiza watumishi wote wanaotuhumiwa kuhusika na ubadhilifu wa zaidi ya
shilingi bilioni tatu wakamate na kuchukuliwa hatua za kisheria na tayari
watumishi saba akiwemo aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbogwe, Carlos
Gwamagobe wamekamatwa kwa ajili ya uchunguzi kuhusiana na ubadhilifu huo.
Aidha akiwa
wilayani Mbogwe, Majaliwa alimuagiza Mkuu wa Mkoa Geita, Mhandisi Robert
Gabriel kumsimamisha kazi aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Mbogwe, Adam
Nyoni ambaye amehamishiwa Halmashauri ya Nyang’hwale ili akajibu tuhuma za
ubadhilifu wa shilingi milioni 19.4 za mfuko wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).
Tazama Video hapa chini
No comments:
Post a Comment