Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizundua Kongani ya tatu ya Centre Limited (SCL) Sagcot-Kilombelo katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Flomi mjini Morogoro tarehe 23 Novemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo)
Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizundua Kongani ya tatu ya Centre Limited (SCL) Sagcot-Kilombelo katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Flomi mjini Morogoro tarehe 23 Novemba 2018.
Mkurugenzi Mtendaji wa SAGCOT Ndg Geofrey Kirenga akieleza mwelekeo wa jinsi SAGCOT itakavyoendesha shughuli zake wakati wa uzinduzi wa Kongani ya tatu ya Centre Limited (SCL) Sagcot-Kilombelo katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Flomi mjini Morogoro tarehe 23 Novemba 2018.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kongani ya tatu ya Centre Limited (SCL) Sagcot-Kilombelo katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Flomi mjini Morogoro tarehe 23 Novemba 2018.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa Kongani ya tatu ya Centre Limited (SCL) Sagcot-Kilombelo katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Flomi mjini Morogoro tarehe 23 Novemba 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Albert Chalamila akitoa ushuhuda toka kongani ya Ihemi na Mbarali wakati wa uzinduzi wa Kongani ya tatu ya Centre Limited (SCL) Sagcot-Kilombelo katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Flomi mjini Morogoro tarehe 23 Novemba 2018.
Muwakilishi wa Benki ya Dunia Bi Emma Isinika Modamba akiwasilisha taarifa fupi toka kwa wadau wa Maendeleo wanaowezesha mpango wa SAGCOT wakati wa uzinduzi wa Kongani ya tatu ya Centre Limited (SCL) Sagcot-Kilombelo katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Flomi mjini Morogoro tarehe 23 Novemba 2018.
Na Mathias Canal, Wizara ya
Kilimo-Morogoro
Mageuzi ya kilimo nchini Tanzania yanapaswa kutiliwa mkazo na wadau wote
wa sekta ya kilimo wakiwemo wananchi, wadau wa maendeleo na serikali kwa
ujumla.
Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo tarehe 23
Novemba 2018 wakati akizundua Kongani ya tatu ya Centre Limited (SCL) Sagcot-Kilombelo
katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Flomi mjini Morogoro.
Mhe Hasunga alisema kuwa Sekta ya kilimo imeendelea kuwa uti wa mgongo
wa uchumi wa Tanzania kwani imekuwa ikichangia kwa Kiasi kikubwa katika kutoa
ajira, kuchangia karibu nusu ya mauzo yote ya nje na hivyo kuchangia kwa kiasi
kikubwa katika kuleta fedha za kigeni.
Alisema kuwa Serikali imeendelea kuweka juhudi zake katika kuwezesha
sekta ya kilimo kwa kufanya mabadiliko mbalimbali ya kisera yenye lengo la
kuweka mazingira wezeshi kwa sekta ya kilimo kukua.
Pia serikali imezindua Mpango wa pili wa Maendeleo ya Kilimo (ASDP II)
wenye lengo la kuhakikisha sekta ya kilimo inakuwa na inachangia katika
maendeleo ya uchumi na kuongeza kipato cha mkulima mdogo.
Mhe Hasunga amesisitiza kuwa mpango wa SAGCOT ulianza toka mwaka 2010
kwenye mkutano wa Baraza la Uchumi la Dunia kwa Africa (World Economic Forum of
Africa WEF-A) uliofanyika Jijini Dar es Salaam ambao utatekelezwa kwa miaka 20
mpaka mwaka 2030.
Alisema mpango wa SAGCOT umepangwa kutekelezwa kwa awamu katika mgawanyo
wa kongani sita. Kongani hizo Ihemi, Mbarali, Kilombero, Rufiji, Ludewa na
Rukwa hivyo ili kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao ameitaka SAGCOT kuongeza
ufanisi na weledi katika kukamilisha kongani zote sita kama mtazamo ulivyo.
Naye Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba akizungumza katika hafla
hiyo alisema kuwa wizara ya kilimo ina ziada ya kutosha kwenye mazao ya chakula
huku akisisitiza kuwa mkakati wa kutafuta masoko unaendelea ili kuwanufaisha
wakulima nchini.
Alisema nchi ina fursa kubwa kwenye sekta ya kilimo hivyo wananchi
wanapaswa kujikita zaidi katika kilimo kwani ndio sehemu pekee yenye uwezo wa
kuwanufaisha wananchi wengi kwa wakati mmoja.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa alisisitiza kuwa SAGCOT
inapaswa kufanya haraka katika kuanzisha kongani ya nne na hatimaye mpaka ya
sita ili kuajiri vijana na wananchi wengi.
Ameongeza kuwa wataalamu wengi wa kilimo wamenufaika na elimu nchini
lakini ajira zimekuwa chache hivyo kuongezwa kwa kongani nyingine ajira
zitaongezeka na wananchi wengi watanufaika na kipato kwa ajili ya maendeleo ya
kaya na Taifa kwa ujumla wake.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa SAGCOT Ndg Geofrey Kirenga
alieleza kuwa malengo ya mpango wa SAGCOT yanakwenda sambamba na Dira ya
maendeleo ya Taifa ya 2025, mpango wa maendeleo wa miaka 5, utekelezaji wa
mpango wa pili wa maendeleo ya kilimo (ASDP II) na mpango wa uwekezaji kwenye
kilimo kwa ajili ya usalama wa chakula na lishe (TAFSIP) ambao unatumika
kutekeleza programu kabambe ya maendeleo ya kilimo barani Afrika (CAADP).
Alitaja lengo kuu la mpango wa SAGCOT kuwa ni kuhakikisha kuwa kilimo
katika maeneo ya SAGCOT kinachangia katika kuongeza tija, kuhakikisha kuna
usalama wa chakula, kupunguza umaskini, kuhakikisha wakulima wadogo wanatoka
kwenye kilimo cha kujikimu na kwenda kwenye kilimo cha kibiashara na
kuhakikisha mazingira yanatuzwa kwa maendeleo endelevu ya kilimo.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment