Sunday, November 25, 2018

CHAMA CHA MAPINDUZI CHASISITIZA UTOLEWAJI WA MIKOPO ISIYOKUWA NA RIBA ILI KUWAINUA WANANCHI KIUCHUMI

25 Novemba 2018

Katika kongamano la vijana na Uchumi lililoandaliwa na Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Vijana House of Vision lililofanyika tarehe 24-25 Novemba 2018 katika Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni, Dar es salaam Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndg polepole anasema Chama Cha Mapinduzi kinasisitiza utolewaji  wa mikopo  isiyokuwa na riba ili kuwainua wananchi kiuchumi.

Akihutubia kwa mamia ya vijana waliohudhuria kongamano hilo Ndugu Polepole amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali yake itahakikisha inashirikiana Asasi za Kiraia zenye dhamira ya kuwezesha wananchi na wajasiriamali kufanikisha malengo waliojiwekea ya kuinuka kiuchumi.

Ilani ya CCM ya uchaguzi 2015-2020 katika fungu LA 56 inazungumzia juu ya uwezeshaji wananchi kiuchumi hivyo lazima ipatikane namna nzuri na rahisi ya kuwawezesha wajasiriamali ili kuweza kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali ya Awamu ya Tano alisema Ndg Polepole

Aidha Ndg Polepole amesisitiza wajasiriamali kupata elimu sahihi na kuzingatia shughuli za ujasiriamali zenye tija, kutumia mtaji kidogo kwa  matokeo makubwa pamoja  na kuchangamkia fursa zinazotolewa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Ndugu John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 🇹🇿 katika kuwezesha wananchi wake kiuchumi.

Huu ni muendelezo wa Kazi Chama nje ya Chama  ndani ya Jamii na katika kuhakikisha malengo yaliyowekwa na Serikali ya CCM ya kuinua wananchi kiuchumi yanafikiwa kwa wakati

Imetolewa na,

IDARA YA ITIKADI NA UENEZI

CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

No comments:

Post a Comment