Thursday, November 29, 2018

Biteko mbele ya Majaliwa- “Ukifika Masumbwe usiongolee madini hueleweki”

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika uwanja wa shule ya Msingi Masumbwe, Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita, jana Novemba 29, 2018.
Tazama Video hapa chini
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa akisalimiana na wakazi wa Kata ya Lulembela (hawako pichani), baada ya kuwasili wilayani Mbogwe kwa ajili ya ziara ya kikazi.
Mkuu wa Mkoa Geita, Mhandisi Robert Gabriel akiwasilisha salamu zake wakati wa ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (hayuko pichani) wilayani Mbogwe.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (hayuko pichani), aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita, zinazojengwa katika Kijiji cha Kasosobe.
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Kasosobe waliojitokeza kumlaki Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akiweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa jengo la ofisi za Halmashauri ya Mbogwe.
Wakazi wa Kata ya Masumbwe wilayani Mbogwe walimlaki Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa picha hii murua kabisa. Na George Binagi-GB Pazzo

No comments:

Post a Comment