Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na waandishi wa habari tarehe 29 Novemba 2018 katika Ukumbi wa Bodi ya Korosho Mjini Mtwara ili kutoa tathmini ya hatua zilizofikiwa na serikali za ununuzi wa korosho za wakulima. (Picha Zote Na Mathias Canl, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na waandishi wa habari tarehe 29 Novemba 2018 katika Ukumbi wa Bodi ya Korosho Mjini Mtwara ili kutoa tathmini ya hatua zilizofikiwa na serikali za ununuzi wa korosho za wakulima.
Na Mathias Canal,
Wizara ya Kilimo-Mtwara
Serikali imetangaza kuongeza kasi ya malipo ya wakulima wa
Korosho ili kufikia kiasi cha shilingi Bilioni nne (4) au zaidi kila siku kwani kufanya
hivyo zoezi la malipo kukamilika haraka.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo
tarehe 29 Novemba 2018 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi
wa Bodi ya Korosho Mjini Mtwara ili kutoa tathmini ya hatua zilizofikiwa na
serikali za ununuzi wa korosho za wakulima.
Amesema kuwa zoezi hilo litaenda sambamba na kuongezwa kwa
wataalamu kwa ajili ya kuongeza nguvu ya malipo huku akisisitiza kuwa wataalamu
wengine tayari wamekuwa na uzoefu wa namna ya kuhakiki na namna ya kulipa tangu
kuanza kwa zoezi hilo.
Mhe Hasunga alisema kuwa mikoa inayolima korosho ni mingi
nchini hivyo wakati tathmini sambamba na malipo zikiendelea timu ya wataalamu
wengine itaundwa kwa ajili ya kuanza kufanya tathmini katika mkoa wa Pwani na
mikoa mingine inayolima korosho nchini.
Katika hatua nyingine amesema kuwa serikali imejipanga kuwatambua
wakulima wote wa korosho nchini ili kurahisisha kuwahudumia na kuainisha
tathimini mahususi ya wakulima hao nchini.
Kuwafahamu wakulima hao itaisaidia serikali namna ya
kushirikiana nao na kuwasaidia ili wakulima hao waweze kuongeza uzalishaji na
tija katika kilimo.
Miongoni mwa changamoto ilizokutana nazo serikali katika
zoezi la uhakiki ni pamoja na kutotolewa takwimu sahihi na Vyama vya msingi vya
ushirika za wakulima wa korosho kwani takwimu hizo zinatofautiana na vyama
vikuu vya ushirika.
“Jambo hili la takwimu kwenda kinyume linatupa uhakika kwamba
kuna taarifa zilikuwa zinapikwa ili kumnyonya mkulima lakini changamoto zingine
ambazo zimetukumba ni pamoja na uchache wa maghala kwani yaliyopo hayatoshi”
Alikaririwa Mhe Hasunga
“Kuna changamoto za mgomo wa wapakuaji na wapakiaji wa mizigo,
nasi kama serikali tutakuwa na kikao hivi karibuni na wasafirishaji ili
kuhakikisha kuwa wanalipwa fedha zao haraka iwezekanavyo baada ya kupitia
mikataba yao kujiridhisha jinsi walivyokubaliana” Alisema
Tayari vyama 163 vya wakulima wa korosho vimekwisha hakikiwa mpaka
kufikia jana jioni tarehe 28 Novemba 2018 kati ya vyama 617 vinavyojihusisha na
zao la korosho nchini.
Katika vyama hivyo vilivyohakikiwa tayari malipo yamevifikia
vyama 97 ambapo wakulima 22,269 wameshalipwa huku kiasi cha korosho ambazo zimekwishalipiwa
ni kilo 6,712,681 huku jumla ya Bilioni 22,151,00,000.8 zikiwa zimekwishalipwa.
Aidha, mpaka kufikia jana jioni tarehe 29 Novemba 2018
serikali imekwisha hamisha kiasi cha Tani 9,347.2 kutoka kwenye maghala makuu.
Pia Waziri Hasunga ameyataja matarajio ya serikali katika
uzalishaji wa Korosho kuwa ni takribani Tani 245,495.8
MWISHO
No comments:
Post a Comment