Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
mh. Joachim Wangabo amemtaka Mkurugenzi wa Halmauri ya Wilaya ya Sumbawanga
kuhakikisha anahamishia ofisi zake karibu na wananchi ambao wanishi katika
mipaka ya halmashauri yake na sio kubaki mjini.
Amesema kuwa kwa kufanya
hivyo mji utatanuka na maendeleo yatapatikana na pia kupunguza gharama za
kuwahudumia wananchi pindi majanga yanapotokea kwani kuwa nao karibu
kutasababisha kutotumia pesa nyingi kuwafuata na wao kupata urahisi wa kufika
katika ofisi hizo.
“Rai yangu mkurugenzi
mtafute mahala kwingine kwa kujenga ofisi za halmashauri ya wilaya, mahala
pengine ambapo ni ndani ya halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga na sio ndani ya
manispaa, ofisi hii inapaswa iwe nje ya eneo la manispaa, faida yake ni kupanua
huduma kuliko kila kitu kufikiria manispaa,” Alisema
Ameyasema hayo
alipokwenda kukagua jengo jipya la halmashauri hiyo ambalo lilianza kujengwa
mwaka 2012 na kutegemewa kumalizika mwaka 2013 japokuwa bado kukamilika ambapo
serikali ilitenga shilingi bilioni 2.3 lakini hadi kufikia katika hatua ya
sasa, tayari shilingi bilioni 1.6 zimeshatumika kupitia fedha za Ruzuku ya
Miradi ya Maendeleo (CDG) ambapo kwa sasa imefutwa.
Awali akitoa taarifa ya
jengo hilo Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga John Msemakweli amesema
kuwa halmashauri tayari imekwisha tuma andiko maalum na kupeleka wizara ya
fedha na OR – TAMISEMI ili kuwezeshwa kumalizia jengo hilo litakalokuwa na
ofisi 76 na kumbi 2.
“Hadi sasa tumeandika
andiko maalum la jumla ya shilingi 716,933,989 ili kukamilisha mradi huu,
tunategemea jengo hili likikamilika litakuwa na ofisi 76 na kumbi 2 ambazo
zitakuwa zinatosheleza mahitaji ya ofisi za watumishi wote walio katika makao
makuu ya Halmashauri ya Wilaya,” Alibainisha.
Jengo hilo ambalo lipo
karibu na jengo la Manispaa ya Sumbawanga halijatengewa fedha za kuliendeleza
tangu mwaka wa fedha 2015/2016 hadi sasa.
Katika hatua nyingine,
Mh. Wangabo alimuagiza Mkurugenzi huyo kuunda timu ya kuhakikisha wanapambana
na mifugo inayoharibu barabara kwani serikali inatumia mabilioni kuzitengeneza
na kuzikarabati na hivyo si vyema uharibifu huo ukaendelea.
No comments:
Post a Comment