Wednesday, October 3, 2018

NAIBU WAZIRI OR-TAMISEMI AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA KITUO CHA AFYA CHA KISASA KIMARA

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe Josephat Sinkamba Kandege leo amefanya Ziara Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam.

Katika ziara yake iliyoanzia ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori Kibamba CCM Mhe Naibu Waziri OR-TAMISEMI alipata wasaa wa kufanya mazungumzo na Mkuu wa Wilaya Mhe Kisare Makori

Katika Mazungumzo hayo Mhe Kisare Makori alimuhakikishia  Mhe Naibu Waziri OR-TAMISEMI Ubungo ni salama wakazi wake wako salama wanaendelea vizuri na majukumu yao ya kila siku.

Mhe Kisare Makori akasema zipo changamoto ndogondogo za wafanyabiashara wadowadogo wanaofanya biashara barabarani lakini ofisi yangu pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa tumejipanga kuhakikisha wafanya biashara hao wanatengewa maeneo rasmi ya kufanya biashara zao.

Baada ya hapo Mhe Kisare Makori akamueleza Mhe Naibu Waziri OR-TAMISEMI kuhusiana na ujenzi wa kituo cha afya Kimara na ndipo timu ya wataalamu wakiongozwa na Mkurugenzi Bi Beatrice Dominic pamoja na timu ya ofisi ya mkuu wa Wilaya na Mhe Naibu Waziri OR-TAMISEMI ikaanza ziara kutembelea kituo hicho.

Mhe. Naibu Waziri OR-TAMISEMI Mhe*Josephat Sinkamba Kandege* alipozuru katika kituo cha afya kimara akakagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho akahimiza ujenzi wa kituo hicho uzingatie utojiaji huduma zinazoendana na Hospitali (sem-hospital).

"Nataka kituo hiki kikikamilika kitoe huduma zote muhimu za afya ambazo zinaendana na Hospitali wakazi wa Ubungo wasipate shida kabisa za matibabu" alisema Mhe Naibu Waziri OR-TAMISEMI.

Aidha Mhe Naibu Waziri OR-TAMISEMI alisema nimekuwa nikiombwa na Mbunge Said Kubenea siku zote Sinza Palestina iwe Hospital ya Wilaya lakini ninachoweza kusema litafutwe eneo ambalo Hospitali ya Wilaya itajengwa.

Na ndipo Mhe Kisare Makore Mkuu wa Wilaya ya Ubungo akasema jitihada zinafanyika za kulitwaa eneo ambalo hospitali ya Wilaya ya Ubungo itajengwa kwa ajili ya ustawi wa watu wetu.

Mwisho akiwa katika eneo ambalo kituo hicho kinajengwa aliweza kuzungumza na viongozi wa kisiasa wa Chama Dola CCM pamoja na Diwani wa kata hiyo lakini pia Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob.

Wote kwa umoja wao wakawa na kauli moja kwenye suala la maendeleo utofauti wa itikadi unakuwa pembeni kama Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli anavyosema maendeleo kwanza vyama badae.

Imetolewa na:
kitengo cha Habari na Uhusiano
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

No comments:

Post a Comment