Mkurugenzi wa Mnaispaa ya Sumbawanga Jacob Mtalitinya ameondoa
sintofahamu iliyokuwa imesambaa katika manispaa hiyo juu ya maagizo na
maelekezo mablimbali aliyoyatoa katika kuboresha huduma kwa kukusanya mapato na
kumsaidia mwananchi mmoja mmoja kujiboreshea maisha katika manispaa hiyo.
Mtalitinya alisema kuwa sula la vibali vya ujenzi na leseni za
makazi imetafsirika tofauti lakini azma ni kuipima Manispaa kwa asilimia 100 na
kuwa huo ni mwendo wa kufanya upimaji.
Tangu kuwasili kwa Mkurugenzi huyo mapema mwezi wa nane mwaka
huu wananchi wengi wamekuwa wakipotosha maelekezo anayoyatoa na matokeo yake
kueleweka vibaya kwa wananchi wengi wa Manispaa ya Sumbawanga.
“Unapotaka kujenga jengo lako, unashauriwa kuepuka
usumbufu, upate kibali kutoka ofis ya Mkurugenzi na utaratibu wa jengo
utakaolifanya, tumeweka nguvu sana kwenye kata za mjini lakini haimaanishi hata
kata hizi za pembezoni hazitakiwi kutii sheria hiyo. Leseni ya makazi
tunakusudia kuipima Manispaa yetu kwa asilimia 100,” Alibainisha.
Pia alizitaja faida za leseni ya makazi ikiwa ni pamoja na kuwa
mmiliki halali wa eneo, kurasimisha makazi ili kupata huduma za msingi kama
vituo vya afya, barabara na maeneo ya wazi pamojanna kupata hatimiliki
itakayodumu kuanzia mika 33 hadi 99.
Ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika soko
la Kaswepepe, kata ya Sumbawanga Asilia, Wilayani Sumbawanga jambo ambalo
lilipendezwa na wananchi waliohudhuria katika mkutano huo na hatimae kuelewa
lengo la Mkurugenzi.
Mmoja wa wananchi waliohudhuria Ditmali Mwageni alisema kuwa
walishangazwa na kitendo cha mkurugenzi huyo kuwaamuru watu kupaka rangi mabati
kulingana na maagizo ya kila kata kuwa na rangi yake, lakini kwa ufafanuzi
alioutoa nadhani ameeleweka vyema na wananchi waliohudhuria.
“Kusema kwake kuwa agizo hilo linawahusu wale tu ambao wanaanza
kujenga sasa, hapo tumeelewa kuliko tulivyokuwa tunasikia kwamba watu wote
wapake rangi za mabati kulingana na rangi ya kila kata, kwakuwa tu ni agizo la
mkurugenzi, hiyo haikuwa sawa, nyumba zenyewe za zamani, mabati yamechoka,
utekelezaji wake ungekuwa mgumu, lakini kama katoa miaka mitano Kwetu basi
sawa,” Alisema.
Miongoni mwa masuala yaliyozua mzozo ni agizo la kila kata kuwa
na rangi yake ya bati, kupata kibali cha ujenzi kabla ya kuanza ujenzi, kuwa na
leseni ya makazi pamoja na mazoezi mbali mbali ya upimaji yanayoendelea katika
manispaa hiyo.
No comments:
Post a Comment