Na Mathias Canal, Kigali-Rwanda
Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba amemaliza majukumu ya kikazi mjini Kigali nchini Rwanda ambapo pamoja na mambo mengine amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Rwanda Mhe Ernest Mangu kabla ya kurejea nchini Tanzania.
Mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Kigali Conversion Centre yalijikita katika kuinua zaidi mahusiano ya Rwanda na Tanzania hususani katika sekta ya kilimo, ikiwa ni mara baaa ya kumalizika siku nne za Kongamano la Mapinduzi ya kijani Barani Afrika (AGRF 2018).
Waziri Tizeba amempongeza Balozi Mangu kwa kazi kubwa ya kuendeleza mahusiano chanya kati ya nchi hizo mbili huku akimsihi kuongeza ufanisi zaidi kwa manufaa ya wananchi katika nchi hizo za (Rwanda na Tanzania).
Naye Balozi Mangu ametoa pongezi kwa Waziri huyo mwenye dhamana ya kilimo nchini Tanzania kwa usimamizi madhubuti wa sekta ya kilimo hususani usimamizi uliotukuka kwenye Ushirika.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment