Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba, Waziri wa kilimo akitoa ufafanuzi kuhusu zao la kahawa wakati akiwasilisha taarifa ya mwenendo wa soko la kahawa nchini kwa Dkt Bashiru Ali Kakurwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi mkutano uliohudhuriwa na wabunge kutoka maeneo yote yanayozalisha kahawa, Jana Tarehe 14 Septemba 2018 katika ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi maarufu White House Mjini Dodoma. (Picha Zote Na Mathias Canal, WK)
Washiriki wa mkutano wa uwasilishaji wa mwenendo wa zao la kahawa wakifatilia kwa makini taarifa iliyowasilishwa na Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba, Waziri wa kilimo mbele ya Dkt Bashiru Ali Kakurwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi mkutano uliohudhuriwa na wabunge kutoka maeneo yote yanayozalisha kahawa, Jana Tarehe 14 Septemba 2018 katika ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi maarufu White House Mjini Dodoma.
Dkt Bashiru Ali Kakurwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi akizungumza mara baada ya Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba, Waziri wa kilimo kutoa ufafanuzi kuhusu zao la kahawa wakati akiwasilisha taarifa ya mwenendo wa soko la kahawa nchini, Jana Tarehe 14 Septemba 2018 katika ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi maarufu White House Mjini Dodoma.
Dkt Bashiru Ali Kakurwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (Wa pili kushoto) akiendesha kikao mara baada ya uwasilishwaji taarifa ya mwenendo wa soko la kahawa nchini, Jana Tarehe 14 Septemba 2018 katika ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi maarufu White House Mjini Dodoma. Wengine ni Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba, Waziri wa kilimo (Kushoto), Naibu waziri wa kilimo Mhe Omary Mgumba (wa kwanza kulia) na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga (wa tatu kulia)
Wataalamu kutoka wizara ya kilimo wakifatilia mkutano wa uwasilishaji wa mwenendo wa zao la kahawa taarifa iliyowasilishwa na Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba, Waziri wa kilimo mbele ya Dkt Bashiru Ali Kakurwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi mkutano uliohudhuriwa na wabunge kutoka maeneo yote yanayozalisha kahawa, Jana Tarehe 14 Septemba 2018 katika ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi maarufu White House Mjini Dodoma.
Na Mathias Canal-WK, Dodoma
Katika
vipindi mbalimbali vya historia ya Tanzania masoko ya Kahawa yamekuwa
yakiendeshwa kwa mfumo wa ushirika na soko huria, Mfumo wa soko huria uliruhusu
makampuni na watu binafsi kununua mazao moja kwa moja kutoka kwa wakulima
pasipo udhibiti hali iliyopelekea kuwepo kwa changamoto mbalimbali zikiwemo bei
isiyokuwa na tija kwa mkulima, ubora hafifu wa mazao, ukwepaji wa kodi kwa
wanunuzi na ukosefu wa takwimu sahihi za uzalishaji na mauzo.
Kutokana
na changamoto za mfumo wa soko huria, Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na
Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli iliamua
kurejesha ununuzi wa mazao matano ya kimkakati (Korosho, Tumbaku, Pamba,
Kahawa, na Chai) kupitia vyama vya ushirika tangu mwaka 2016 ili kunufaisha
wakulima, wanunuzi/wafanyabiashara na serikali.
Hayo
yamebainishwa jana tarehe 14 Septemba 2018 na Mhandisi Mhe Dkt Charles Tizeba,
Waziri wa kilimo wakati akiwasilisha taarifa ya mwenendo wa soko la kahawa
nchini kwa Dkt Bashiru Ali Kakurwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi katika
ukumbi wa mikutano wa CCM Makao makuu maarufu kama White House, Mkutano
uliohudhuriwa na wabunge kutoka maeneo yote yanayozalisha kahawa, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu
Ngemela Lubinga, Mjumbe
wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (NEC) Makongoro Nyerere, Naibu
waziri wa Kilimo, Mhe Omary Mgumba, wataalamu kutoka wizara ya kilimo akiwemo
Naibu katibu mkuu Prof Sizya Tumbo, Mrajis wa vyama vya ushirika,vyama vya
ushirika na wawakilishi wa wakulima kutoka maeneo yanayolima kahawa.
Katika
taarifa hiyo Dkt Tizeba alieleza kuwa kamwe hawezi kuruhusu mtu mmoja mmoja au
kundi la watu kuvunja ushirika ambao hivi karibuni umeanza kuimarika mahususi
kwa ajili ya kumkomboa mkulima uamuzi ambao umebainishwa kwenye ilani ya
uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020 katika sura ya pili ibara ya
22 ikisisitiza kuviimarisha na
kuviwezesha vyama vya ushirika kuwa na uwezo wa kutafuta masoko ya mazao ya
wakulima ya ndani na nje kwa kuweka mfumo madhubuti wa ukusanyaji, uchambuzi na
uenezaji wa taarifa za masoko na kutoa elimu juu ya uongezaji wa thamani na
biashara.
Alieleza
kuwa zipo faida nyingi kwa mkulima anapouza kupitia ushirika na hasa vyama vya
msingi ambazo ni pamoja na wakulima kuwa na nguvu ya pamoja ya kushauriana ili
kupata bei nzuri na kunufaika na kilimo, wakulima kupata nguvu ya kuanzisha na
kuendesha maghala na viwanda vya kuongeza thamani ya mazao yao, kuwawezesha
wakulima kutunza ubora wa mazao kwa mujibu wa sheria, kanuni na miongozo ya
mazao husika.
Faida
zingine ni kuwawezesha wakulima kupunguza gharama za uzalishaji kwa kuagiza pembejeo
kwa pamoja, kuwezesha upatikanaji mazao ya uhakika na yenye ubora kwa wanunuzi,
kuwezesha serikali za mitaa na serikali kuu kupata mapato yake stahiki
kulingana na uzalishaji halisi, kuwezesha upatikanaji wa takwimu sahihi za
idara ya wakulima na uzalishaji; na kuwawezesha wanunuzi kufanya malipo ya
mazao kwa kuzingatia makubaliano yaliyofikiwa katika minada.
Aidha,
Dkt Tizeba alisema kuwa mwenendo wa mauzo ya kahawa kwa msimu wa mwaka
2016/2019 ni mzuri ukilinganisha na misimu miwili iliyopita ya mwaka 2016 na
2017. Mauzo ya kahawa kwa mwezi Agosti 2018 ni mara mbili ya mauzo ya msimu wa
mwaka 2017 ni mara nne ya msimu wa mwaka 2016. “Mauzo ya kahawa mwezi Septemba
2018 kwa mnada mmoja uliofanyika ni zaidi ya mauzo yote ya mwezi Septemba 2017
na ni sawa na mauzo yote ya kahawa kwa mwezi Septemba msimu wa mwaka 2016”
Alisisitiza Dkt Tizeba
Kwa
upande wake Dkt Bashiru Ali Kakurwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi
akizungumza mara baada ya mjadala huo kutuama kwa masaa 8 kujadili namna ya
kupata masoko ya mazao ya kilimo, urahisi wa upatikanaji wa mitaji, siasa ya
kilimo kupitia ushirika na maandalizi ya miundombinu rafiki katika kilimo,
alisema kuwa nchi ya Tanzania ipo katika mageuzi makubwa ya kimfumo na kimuundo
hivyo mgogoro wa kiuchumi ni lazima ujitokeze kutokana na watu kulazimisha
mazoea na haramu kuwa halali.
Alisema
kuwa viongozi wote wa chama na serikali wanapaswa kuunga mkono jitihada za
serikali kumkomboa mkulima kupitia ushirika, kujenga uchumi kupitia mshikamano lakini
ushirika unaotakiwa ni ule wa Demokrasia wenye mizizi imara ili kuimarisha
usalama wa nchi katika kilimo ambao unategemea wakulima wadogo.
Dkt
Bashiru aliongeza kuwa ni lazima CCM kiwe chama kinachoingoza na kuisimamia
serikali kwa kujenga utamaduni wa kujadiliana mambo muhimu ya kitaifa ili
kukifanya chama hicho kuongeza imani maradufu kwa wananchi waliokiamini chama
hicho na kukipa dhamana ya kuongoza Dola kupitia ilani ya ushindi ya mwaka
2015-2020.
Katika
hatua nyingine ameitaka Wizara ya kilimo na Wizara zingine zote sambamba na
taasisi za umma kutoa taarifa za mara kwa mara kwenye vyombo vya habari kuhusu
yale yanayofanywa na serikali, kueleza mikakati ya serikali katika kuimarisha
uchumi, sambamba na kutaja mafanikio yanayofanywa na serikali ili kuongeza
uelewa kwa wananchi ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakipotoshwa.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment