Saturday, August 4, 2018

NAIBU WAZIRI ANGELINA MABULA AUPONGEZA MRADI WA LTA MKOANI IRINGA

Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina Mabula akitoa maelezo kwa uongozi wa mradi wa LTA mkoani Iringa jinsi ya kuutekeleza na kuwafika wananchi wa wilaya ya Iringa.
Meneja mradi wa urasimisha ardhi LTA Mustafa Issa  akitoa maelezo jinsi gani wanavyotekeleza mradi huo na kutumia teknolojia ya simu maalufu kama MAST
Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina Mabula akiwa makini kusikiliza jinsi teknolojia ya MAST inavyotumika katika upimaji wa ardhi kwa wananchi
Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina Mabula akiwa na viongozi mbalimbali wakipata maelezo ya jinsi hati za kimila zinavyotengenezwa kwa kupitia mradi wa MAST

NA FREDY MGUNDA IRINGA.

Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina Mabula aliwataka viongozi wanaosimamia mradi wa kurasimisha ardhi LTA kuhakikisha wanapima vijiji vyote vya wilaya ya Iringa.

Akizungumza na viongozi pamoja na wafanyakazi wa mradi wa LTA Naibu waziri Mabula alisema wananchi wakipimiwa ardhi zao zitaongeza thamani ya maisha na kuongeza maendeleo.

“Kwasasa sasa mmepima vijiji vichache sana hivyo mnatakiwa kuongeza kuhudi na kutuma maombi kuhakikisha mnapima vijiji vyote vya wialaya ya Iringa ili kuongeza thamani ya ardhi” alisema Mabula

Mabula aliupongeza mradi wa mradi wa urasimisha ardhi LTA na kusema kuwa serikali itakikisha inashikiana vizuri ili kupunguza migogoro ya ardhi kwa wananchi kote nchi kwa kutumia miradi ambayo inafanya vizuri kama huu.

“Nimeona mradi huu wa LTA unavyofanya vizuri hivyo iwechachu ya kwenda kupima vijiji vyote ili ili kumaliza migogoro kwa wananchi na kuhakikisha kuwa wananchi wanajua umuhimu wa kutunza na kuthamini ardhi hapa nchini” alisema Mabula

Aidha Mabula ameupongeza mfumo wa teknolojia ya MAST ambayo imerahisiha upimaji wa ardhi katika vijiji mbalimbalia hapa nchini na kuwaomba viongozi na wizara kuhakikisha mashirika ambayo yanajihusisha na upimaji wa ardhi kuja kujifunza teknolojia hii.

Naye meneja mradi wa urasimisha ardhi LTA Mustafa Issa alisema kuwa mradi huu umesaidia kutatua migogoro mingi ya wananchi wa wilaya ya Iringa.

Kwenye vijiji kulikuwa na migogoro mingi sana juu ya umiliki wa ardhi lakini kupitia mradi huu tumefanikiwa kutatua kero nyingi sana za ardhi.

No comments:

Post a Comment