Thursday, August 2, 2018

MBUNGE JIMBO LA NYAMAGANA KUSIMAMIA KIDETE KERO YA ARDHI KIPINDI CHA UONGOZI WAKE



Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe Stanslaus Mabula adhamilia kusimamia utatuzi wa kero za ardhi kuisha katika kipindi chote cha uongozi wake.

Mhe Mabula amepokea maswali 18 ya wananchi wa Kata ya Mbungani hivi leo katika mkutano wa hadhara wa wananchi eneo la Nyanshana ikiwa maswali 14 yote aliyoyapokea ni kero za urasimishaji makazi, upimaji shirikishi pamoja na migogoro ya ardhi.

Mhe Mabula amewambia wananchi anatambua muingiliano wa baadhi ya ardhi katika kata Mbili ya Mbugani na kata ya Isamiro, hivyo kukabiliana na changamoto hiyo  tayari amezungumza na watalamu wa Mipango Miji na Ardhi katika halmashauri ya Jiji la Mwanza, ambapo wamedhamiri kuondoa kero za ardhi na kuhakikisha swala la urasimishaji maeneo kupitia zoezi  la upimaji shirikishi utafanyika kwa kila kipande cha ardhi cha maeneo ya makazi ambacho hakijapimwa kinapimwa katika Mitaa ya Nyanshana na Kasuru.

Katika sekta ya elimu kupitia mfuko wa Jimbo pamoja na wadau wa maendeleo Mhe Mabula amendelea na uboreshaji wa miundombinu ikiwa ni pamoja na ujenzi wa madarasa na tayari ujenzi wa matundu 20 ya vyoo yamekusudiwa kujengwa.

Mhe Mabula amesema Serikali imejipanga katika mwaka ujao wa fedha imedhamili kuwa na ujenzi wa barabara ya Mawe kutokea Nyanshana Shule ya Msingi kuelekea mpaka wa Ilemela Makaburini. Na tayari inajenga barabara kwa kiwango cha Mawe ya  Dkt Migiro inagharimu shilingi Bi 1.1 yenye urefu wa Kil 1.2 itakayo unganisha Kata hiyo na Isamiro.

Mhe Mabula amemalizia kwa kusema serikali imeweka mpango wa uboreshaji miundombinu wa kisima asilia katika eneo la Nyashana, ili kutoa maji safi na salama ikiwa ni maeneo matatu ya kuchotea maji yanawekwa.

Mkutano huo umehudhuliwa na Diwani kata ya Mbugani, Isamiro, Katibu hamasa Chipukizi UVCCM Mkoa wa Mwanza, viongozi wa Chama Cha Mapinduzi pamoja na watendaji wa serikali.

Imetolewa na 
Ofisi ya Mbunge


Jimbo la Nyamagana

No comments:

Post a Comment