Saturday, August 4, 2018

DKT TIZEBA ASIFU MCHANGO WA WAKULIMA, WAFUGAJI NA WAVUVI KUSAIDIA UPATIKANAJI WA MALIGHAFI ZA VIWANDA

Mgeni rasmi-Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akizungumza akihutubia mamia ya wananchi katika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu Jana 3 Agosti 2018 wakati wa sherehe za uzinduzi wa maadhimisho ya 25 ya Nanenane mwaka 2018 ambayo kitaifa yanafanyika mkoani humo. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya kilimo)
Mgeni rasmi-Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akikagua miche ya maembe inayouzwa na mkulima Adam Warioba kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Musoma alipotembelea Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu Jana 3 Agosti 2018 wakati wa sherehe za uzinduzi wa maadhimisho ya 25 ya Nanenane mwaka 2018 ambayo kitaifa yanafanyika mkoani humo. 
Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akizungumza wakati alipotembelea banda la Wizara ya Maliasili na Utalii katika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu Jana 3 Agosti 2018 wakati wa sherehe za uzinduzi wa maadhimisho ya 25 ya Nanenane mwaka 2018 ambayo kitaifa yanafanyika mkoani humo. 
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka akifurahi jambo na wananchi wa mkoa huo mara baada ya kikundi cha ngoma kutumbuiza katika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu Jana 3 Agosti 2018 wakati wa sherehe za uzinduzi wa maadhimisho ya 25 ya Nanenane mwaka 2018 ambayo kitaifa yanafanyika mkoani humo. 

Na Mathias Canal, Wizara ya kilimo-Simiyu

Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba amewapongeza wakulima, Wavuvi na wafugaji kote nchini kwa ufanisi wao katika kazi kwani wameendelea kusaidia upatikanaji wa malighafi za viwanda zinazohitajika huku akisisitiza kuwa sekta hizo ni muhimili muhimu katika ustawi wa Taifa.

Alisema kuwa matarajio ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ni kuhakikisha uwekezaji katika kilimo, ufugaji na uvuvi unakuwa na tija kwa kuzingatia matumizi ya teknolojia za kisasa na kuongeza thamani ya mazao kwa kuzalisha bidhaa kupitia viwanda vidogo, vya kati na vikubwa.

Waziri wa kilimo ameyasema hayo hayo katika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu Jana 3 Agosti 2018 wakati wa sherehe za uzinduzi wa maadhimisho ya 25 ya Nanenane mwaka 2018 ambayo kitaifa yanafanyika mkoani humo.

Alisema kuwa Uwekezaji katika sekta hizo ukiimarishwa utasaidia kwenye matumizi ya teknolojia katika kuzalisha na kuongeza thamani ya mazao kwa kuzalisha na kuongeza thamani ya mazao na hivyo kuweza kuchangia zaidi katika kuongeza pato la Taifa, kuzalisha ajira na maendeleo kwa ujumla.

Alisema kauli mbiu ya maonesho ya nanenane Kitaifa mwaka 2018 inasema “Wekeza katika kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa maendeleo ya Viwanda” inahamasisha kuongeza uzalishaji wa tija ili kuchangia ukuaji wa uchumi na kuifanya nchi iwe ya uchumi wa kati ifakapo mwaka 2025.

Waziri wa Kilimo, Dkt Charles Tizeba amewapongeza viongozi wa Mkoa wa Simiyu, Mara na Shinyanga  kwa kujenga Jengo la Kudumu (Simiyu Exhibition Hall), katika Uwanja wa Maonesho wa Nanenane wa Kanda ya Ziwa Mashariki na kushauri  kanda zote za Maonesho ya nanenane kuiga mfano kwa kanda hiyo,  ili wananchi waweze kupata elimu endelevu katika teknolojia za kilimo sambamba na kutumika kwa Maonesho ya Kitaifa na Kimataifa. 

Alisema kuwa ni mategemeo yake kuwa katika eneo hilo wakulima na wananchi kwa ujumla watapata uzoefu wa kilimo, hivyo kupanua wigo na uelewa wa wakulima huku akiwashauri viongozi wa Mkoa wa Simiyu kuona namna kuhamasisha wafanyabiashara kujenga hoteli maeneo ya jirani na jengo hilo ili kujiandaa na huduma kwa watu watakaokuwa wakifika kwa ajili ya maonesho hayo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema mkoa utaendelea kufanya maonesho ya Teknolojia mbalimbali kila baada ya miezi mitatu katika Jengo hilo,  ili kuwapunguza kazi Watanzania kwenda nje ya nchi kushuhudia maonesho hayo lakini pia kuvutia mataifa pengine kuja nchini kuonesha teknolojia  mbalimbali za kilimo.

MWISHO

No comments:

Post a Comment