KILIMO NI MAISHA!
MPANGO WA KUENDELEZA SEKTA YA KILIMO AWAMU YA PILI (ASDP II), ULIOZINDULIWA RASMI NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
____________________________
01. Kiasi cha Fedha zitakazotolea na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya awamu ya kwanza ni Tshs. Billioni 943.
02. Kiasi cha Fedha kichaahidiwa kutolewa na Washirika ni Tshs. Trillioni 1.9.
03. Kiasi cha Fedha kitakachotumika kutekeleza Mpango kwa Miaka Mitano (05) ya kwanza ni Tshs. Trillioni 13.8.
04. Kipaumbele kwenye MIFUGO ni Maziwa; Nyama ya Ng'ombe; Mbuzi; Kondoo; Kuku; Ngozi; na Samaki.
05. Kipaumbele kwenye MAZAO ni Mpunga; Mahindi; Uwele; Mhogo; Mbogamboga; Matunda; Mazao ya Mafuta kama Alizeti, Ufuta, Nazi, Michikichi, n.k.
06 Maeneo muhimu katika utekelezaji wa mpango huu
(1) Miundo mbinu ya umwagiliaji na vitendea Kazi vya kilimo biashara
(2) Pembejeo na viatirifu vya kilimo biashara kwa ajili ya kuongeza thamani ya kilimo
(3) Masoko na kuongeza thamani kwa kuhamasisha viwanda vidogo na vikubwa kuleta mageuzi ya kilimo
07 Matarajio ya Mpango huu kwa wanachama wa mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (MKIKITA)
(1) Kuongeza chachu yakilimo shirikishi hususani kwenye kilimo cha matunda, mboga, viungo, kilimo maji na ufugaji samaki kibiashara
(2) Kuongeza nyanja mpya ya kilimo bahari (Blue farming). Tanzania Lazima itoke kilimo Kijani kwenda kilimo bahari kwasababu miundo mbinu ya maji ni ndiyo kigezo kikuuu cha kilimo bahari Tanzania tunakila cha kujivunia kwa hilo
(3) Kuongeza thamani mazao kuanzia udongo, viatirifu na mbolea bora ya kuongeza afya na viwanda katika kila hatua ya uzalishaji
(4)Mitaji ya fedha katika mpango huu sio tatizo tena, kwa wanachama wa mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania tunachohitaji ni umoja, utulivu na maarifa ya kufanya Kazi kwani ASDP2 Inafedha ya kutosha kipitia serikali, wadau wa nje, taasisi binafsi za kifefha zimetakiwa kupunguza riba na masharti nafuu pia Mkikita itajenga uhusiano wa karibu mno na serikali kurahisisha uunganishwaji na hizo fursa ya mitaji kupitia mfumo wake wa uwekezaji shirikishi
(5)Masoko. Mpango wa ASDP2 umejenga miundo mbinu rahisi ya kukizi mahitaji ya ndani yaani soko la ndani, mahitaji ya nje yaani ubora na uwiyano wa mzunguko wa mahitaji ya soko la nje na mwisho ni mahitaji ya soko la viwanda
ASDP2 ni jawabu la kilimo biashara Tanzania
No comments:
Post a Comment