Tuesday, June 5, 2018

DC MUWANGO ARIDHISHWA NA UKARABATI CHUO CHA UALIMU NACHINGWEA

Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi Mhe Rukia Muwango ameridhishwa na hatua zilizofikiwa katika ukarabati wa chuo cha ualimu wilayani humo.

Hayo yamejili baada ya Mkuu huyo wa Wilaya  kufanya ziara ya kikazi katika Chuo hicho cha Ualimu Nachingwea, ambapo ameonyesha  kuridhishwa na Ukarabati unaofanywa Chuoni hapo kutokana na  kasi ya ujenzi na thamani ya fedha inayotumika.

Zaidi ya shilingi milioni mia tisa  (900,000,000/=) zimetolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya shughuli hiyo ya ukarabati Mkubwa inayosimamiwa na Mhandisi Mshauri wa Serikali.

Muwango amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe Drkt John Pombe Magufuli kwa yote mema anayowafanyia wananchi katika Wilaya hiyo na Mkoa kwa ujumla.

Alisema kuwa jambo hilo litaongeza chachu na  hamasa ya ufundishaji na ujifunzaji kwa wakufunzi na wanachuo na huku ikiwa sehemu ya  kupendezesha mazingira ya Wilaya hiyo.

Katika hatua nyingine Mhe Muwango aliwaasa Wanachuo kutunza miundombinu hiyo baada ya kukamilika kwa ukarabati huo Mkubwa ambao haujawahi kufanyika tangu chuo hicho kijengwe mwaka 1976.

MWISHO.

No comments:

Post a Comment