Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo akiwa na Mbunge wa Jimbo la Makambako Deo Sanga pamoja na viongozi wengine wakiwa katika ukaguzi wa ofisi za halmashauri ya mji wa makambako.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo akiwapongeza viongozi wa Mji wa Makambako kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa mabweni ya wasichana katika sekondari ya makambako.
Majengo ya halmashauri ya mji wa makambako yanayo endelea kujengwa.
Mbunge wa Jimbo la Makambako Mhe. Deo Sanga pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Jombe. Mhe. Lucy Msafiri wakifurahia jambo wakati wa Ziara ya waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Selemani Jafo Jimboni humo.
..........................................................
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi)Selemani Jafo amezitaka Taasisi za serikali zinazo shughulika na masuala ya ujenzi kuwa kinara kwa ubora wa kazi zinazotekelezwa na taasisi hizo.
Jafo ameyasema hayo leo alipokuwa akikagua ujenzi wa jengo la halmashauri ya Makambako mkoani Njombe linalo jengwa na kampuni ya MZINGA CORPORATION.
Katika ukaguzi huo, jafo ameagiza kazi hiyo ifanyike kwa ubora wa hali ya juu ili kuliwezesha jengo hilo kudumu kwa miaka mingi.
Waziri Jafo kabla ya kukagua ujenzi huo amepata fursa ya kutembelea shule ya sekondari Makambako ambapo serikali imetoa sh.Million 150 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni mawili.
Akiwa katika shule hiyo, Waziri Jafo amefurahishwa na kazi iliyofanywa na halmashauri kupitia kamati ya ujenzi ya shule ambapo mabweni hayo mawili yamekamilika kwa kutumia "Force account'.
Aidha Waziri Jafo amempongeza Mbunge wa Makambako Deo Sanga kwa jitihada kubwa anayo ifanya kuwaletea maendeleo wananchi wake wa Makambako.
No comments:
Post a Comment