Tuesday, May 29, 2018

WIZARA YA ARDHI KUENDESHA MAONESHO YA SIKU TATU VIWANJA VYA BUNGE

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inaendelea na maonesho yake ya siku tangu kuanzia  Mei 28, 2018 katika viwanja vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma yaliyokutanisha wadau mbalimbali wa Ardhi kutoa elimu ya ardhi na mipango miji ili  kurahisisha upatikanaji wa huduma na kuzuia ujenzi holela.

Akizungumza Naibu Waziri wa Wizara hiyo na Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula mara baada ya kutembelea maonesho hayo amesema kuwa wizara imeandaa maonesho hayo ili kuwakutanisha wadau wa Ardhi kwa pamoja ambapo zaidi ya makampuni 30 yamehusishwa ikiwemo Watumidhi House, Makampnu ya Waendelezaji Milki, Makampuni ya Upangaji na Upimaji, Makampuni ya Vifaa vya Ujenzi na Mabenki yanayotoa mikopo ya Nyumba

‘… Kama wizara tumeandaa maonesho yatakayowakutanisha wadau mbalimbali wa ardhi kabla ya kuwasilisha bajeti yetu, nitumie firsa hii kuwaomba waheshimiwa wabunge, wageni waalikwa na watumishi wa bunge  kutembelea maonesho hayo ili kufahamu mambo mengi juu ya ardhi …’ Alisema

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inatarajia kuwasilisha leo bajeti yake kwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ili wabunge  waweze kuijadili na kutoa mapendekezo yao na kisha kuipitisha.

No comments:

Post a Comment