Monday, May 28, 2018

PONGEZI KWA KEISHA KWA KUAMINIWA NA JPM

Katika kikao chake cha kawaida kabisa hii Leo cha Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) kikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kimemteua Khadija Shabaan Taya maarufu kwa jina la Keisha kuwa Mjumbe wa kamati kuu ya Halamshauri kuu ya CCM Taifa (CC). Kipekee nimpongeze kwa moyo mkunjufu kabisa Rafiki na Dada yangu Keisha binafsi nafarijika kwa sababu kubwa mbili, mosi Keisha si mtu wa kukata tamaa lakini pili uwezo anao na ndilo jambo pekee lililonisukuma hata kumpigania kwa kiasi kikubwa wakati anagombea ujumbe wa NEC Mjini Dodoma.

Wakati Mwema...!
Mathias Canal
C.E.O Wazo Huru Media Group
0756413465
Makambako-Njombe

No comments:

Post a Comment