Friday, May 18, 2018

WANANCHI WAIPONGEZA SERIKALI KWA KUIMARISHA MIUNDOMBINU YA AFYA

 Majengo ya Kituo cha Afya cha Sunya kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara yaliyojengwa kwa shilingi milioni 500 zilizotolewa na Serikali.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akiwa pamoja na Waziri wa Ardhi Mhe. Willium Lukuvi wakikagua kituo cha Afya cha Sunya kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akieleza kazi iliyofanyika katika Kituo cha afya cha Sunya kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara kwa  Waziri wa Ardhi Mhe. Willium Lukuvi kwa kutumia shilingi milioni 500 zilizotolewa na Serikali.
Baadhi ya wananchi wa Sunya , Wilayani Kiteto Mkoani Manyara wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo wakati alipotembelea Kituo cha afya cha Sunya kuona maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho.
..................................................
Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara wameipongeza Serikali  ya awamu ya Tano kwa kuhakikisha miundombinu ya afya inaboreshwa na kupunguza malalamiko ya kukosekana kwa huduma ya afya kwa jamii.


Wameyasema hayo wakati wa ziara ya Waziri wa Mchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo alipotembelea  kituo cha afya cha Sunya kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara.



Wananchi hao wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesema Serikali imeweza kutenga bajeti kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa vituo vya afya  208 kwa  lengo la kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya  kwa wakati na karibu na   maeneo wanaoishi.



Wanasema kuwa awali miundombinu mingi ya afya ilikuwa duni, kukosekana kwa vifaa tiba na umbali wa vituo vya afya ilikuwa ni changamoto kubwa kwa jamii hali ambayo ilipelekea wananchi wengi hasa wamama wajawazito kujifungulia nyumbani.



Bw. Muhamed Ally mmoja wa wananchi anaesema awali wanawake walikuwa wakitembea muda mrefu kutafuta huduma za afya na kusababisha vifo vingi vya akina mama wajawazito na watoto chini ya miaka 5, hivyo tunaishukuru serikali kwa kujenga miundombinu ya vituo vya afya nchini.



Wakati huohuo,  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemeni Jafo ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto kwa kusimamia Mradi wa Ujenzi wa mindombinu ya Kituo cha Afya cha Sunya.



Pongezi hizo amezitoa jana wakati alipotembelea kituoni hapo kuona maendeleo ya Miundombinu iliyojengwa kupitia fedha za serikali shilingi milioni 400 kwa ajili ya chumba cha upasuaji, nyumba ya mtumishi, wodi ya mama na mtoto, chumba cha kuifadhia maiti na maabara.


Aidha Mhe.Jafo amesema kwa sasa Serikali imeanza kununua vifaa tiba kwa vituo vyote 208 vilivyokarabatiwa na kujengwa, hivyo amewaomba wananchi wa Sunya kufanya kazi kwa juhudi na maarifa.

No comments:

Post a Comment