Mwandishi wa habari na mchambuzi wa mambo mbalimbali nchini Tanzania Ndg Mathias Canal (Kushoto) akikabidhiwa tuzo ya cheti cha heshima kwa mchango wa utendaji katika jamii na Ndg Mohamed shabani ambaye ni Mkurugenzi wa idara ya jinsia, wazee na watoto wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA).
Mwandishi wa habari na mchambuzi wa mambo mbalimbali nchini Tanzania Ndg Mathias Canal akionyesha cheti cha tuzo ya utambuzi wa utendaji wa kizalendo katika jamii alichokabidhiwa na Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA).
Na Mwandishi Wetu, Dar
es salaam
Mwandishi wa habari na
mchambuzi wa mambo mbalimbali nchini Tanzania Ndg Mathias Canal amepewa tuzo ya
cheti na Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA) ikiwa ni alama ya
kutambua mchango wake na kazi za kizalendo na maendeleo anazozifanya nchini.
Akikabidhi tuzo hiyo kwa
niaba ya Chief Mrindoko Babu Mwidadi ambaye ni Mwenyekiti wa AWAMATA Taifa, Ndg Mohamed shabani Mkurugenzi
wa idara ya jinsia, wazee na watoto wa asasi hiyo ya AMAWATA Taifa amesema
Asasi hiyo imehamasika kutoa tuzo ya cheti cha heshima na pongezi kwa Mathias
Canal kwa sababu ni mzalendo na amekuwa akifikiri juu ya maendeleo ya wananchi
na kuhabarisha wananchi kuhusu mambo mbalimbali ya kimaendeleo na kihabari
jambo ambalo limekuwa ni chachu kwa vijana wengine nchini.
Alisema kuwa Mathias
Canal ni moja ya waandishi wabunifu sana na kama mwandishi kijana amekuwa na
maono makubwa yenye manufaa kwa wananchi na Taifa kwa ujumla, ambapo
amehamasisha vijana wengine kushirikiana nae katika mtandao wake wa Wazo Huru
Blog na WazoHuru.Com chini ya kampuni yake ya habari inayotarajiwa kukamilisha
usajili wake hivi karibuni.
“Tumekuwa tukimfatilia
tangu akiwa Mhariri na mtangazaji wa redio Free Africa (RFA) na baadaye kuwa
mwandishi wa kujitegemea ambapo amefanya kazi na viongozi mbalimbali wa dini,
siasa, jamii na serikali kwa ujumla wake, kwa muda mrefu kama asasi
tumeshawishika kumpa tuzo hii, kwa ufanyaji kazi ya kizalendo na maendeleo hasa
anapoumiza kichwa kwa ajili ya kutengeneza ajira kwa vijana wenzake kupitia
mtandao Wazo Huru Blog" Alikaririwa Mohamed
Akipokea tuzo hiyo,
Mkurugenzi Mtendaji huyo wa Kampuni ya Wazo Huru Media Group (C.E.O), Ndg
Mathias Canal amemshukuru Mwenyekiti wa AWAMATA Taifa Ndg Chief Mrindoko Babu
Mwidadi sambamba na watendaji wote wa Asasi ya AWAMATA kwa kumpatia tuzo hiyo
ya heshima kwani alidhani tuzo hiyo hutolewa kwa viongozi wa serikali pekee.
“Sikufikiria kama
ningeweza kupata heshima hii katika umri wangu huu, kwani nimekuwa nikishuhudia
viongozi mbalimbali wakipewa tuzo hii akiwemo Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo
Ndg John Lipesi Kayombo na hata Mkuu wa Mkoa wa Simiyu kaka yangu Mhe Antony
Mtaka, hivyo hii ni heshima kubwa sana kwangu, imenipa moyo wa kufanya kazi kwa
bidii na weledi zaidi kwa manufaa ya Taifa langu” Alikaririwa Canal
Sambamba na hayo pia
Canal alitoa wito kwa Vijana wenzake kutimiza wajibu wao, katika kusukuma
gurudumu la Taifa mbele ikiwa ni pamoja na kujitokeza katika shughuli
mbalimbali za kijamii sambamba na kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya
tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli.
Asasi ya Wazalendo na
Maendeleo Tanzania (AWAMATA) ni asasi isiyokuwa ya kiserikali
inayojishughulisha na uelimishaji wa uzalendo kwa Watanzania na kufundisha
mbinu za kujitegemea ili kuondokana na umaskini pia inatoa tuzo kwa watu
wanaofanya vizuri katika masuala mbalimbali ya kizalendo na kuwasaidia wananchi
kutoka katika lindi la umasikini.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment