Monday, May 21, 2018

KUMBUKIZI YA AJALI YA MV BUKOBA..!

Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambae pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula inatoa pole na faraja kwa wafiwa na wahanga wa ajali ya Meli ya MV BUKOBA iliyotokea Mei 21, 1996 katika Ziwa Viktoria.

Aidha kupitia Siku hii ( Mei 21, 2018) ya Kumbukizi ya Ajali ya Meli ya MV BUKOBA, Mhe Mbunge anawaasa wasafiri na waendeshaji wa Vyombo vya Usafiri wa  Majini, Nchi Kavu na Angani  kuwa waangalifu na kufuata sheria, taratibu na kanuni ili kuepusha ajali zisizo za lazima.

Pia tunawaomba  wananchi wote kuungana pamoja katika kuwaombea ndugu, jamaa na marafiki tuliowapoteza katika ajali hii.

‘... HAKIKA SOTE NI MAVUMBI NA KWAKE TUTAREJEA  ...’ Zaburi 146.4

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
Mei 21, 2018.

No comments:

Post a Comment