Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringakupitia
chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiongea na viongozi wa misikiti yote ya manispaa ya Iringa wakati wa utoaji sadaka ya tende kwa waumini wa dini ya kiislamu
wa manispaa ya Iringa kwa ajili ya kuadhimisha mfungo wa ramadhan kwa waislamu
wa wote wa manispaa ya Iringa.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza amemshukuru mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati kwa kutoa sadaka ya tunda la tende kwa waiislamu katika kipindi hiki cha mfungo wa ramadhan.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akikabidhi tende alizokabidhiwa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringakupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati kwa kutoa sadaka kwa waiislamu katika kipindi hiki cha mfungo wa ramadhan.
Mkuu wa walimu na msimamizi wa misikiti ya Dhinureyn Tanzania Abdul Salam Ahmad Ayub akimshukuru mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati kwa sadaka aliyoitoa kwa waislam katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhan.
Baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi (CCM) na viongozi wa misiki ya manispaa ya Iringa walipohudhulia zoezi la utoaji wa sadaka ya tende ilitolewa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringakupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati
NA FREDY MGUNDA, IRINGA.
MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Iringakupitia chama cha
mapinduzi (CCM) Ritta Kabati ametoa sadaka ya tende kwa waumini wa dini ya
kiislamu wa manispaa ya Iringa kwa ajili ya kuadhimisha mfungo wa ramadhan kwa
waislamu wa wote wa manispaa ya Iringa
Akizungumza wakati wa kukabidhi sadaka hiyo katika msikiti
wa Dhinureyn Gangilonga Kabati alisema kuwa kila mwaka amekuwa akifutulisha
katika maeneo mbalimbali hivyo mwaka huu ameamua kununua tende na kugawa kwenye
misikiti yote ya manispaa ya Iringa.
“Unajua mwaka huu tende ni tunda ambalo linahitajika katika
kipindi hiki cha mfungo na kuna watu ambao hawana uwezo wa kununua tende hizi
na ukiangalia mwaka huu tende zimepanda bei sana hivyo kwa kiasa ambacho
nakipata nimeamua kutoa sadaka hii kwa waumini wa kiislam” alisema Kabati
Kabati aliwataka wananchi wengine kuendelea kumuabudu
mwenyezi mungu pale ambapo tunapata nafasi ili kupunguza maovu ambayo tumekuwa
tukiyatenda kwa kukusudia au bila kukusudia na kufanya hivyo basi mwenyezi
mungu atatuongezea pale ambapo tumepunguza kwa ajili ya kumtumiaka mungu.
“Katika kipindi hiki nawaomba wazazi,walezi na viongozi
wetu naomba tutoe elimu kwa vijana wetu kwa kuwapa elimu ya dini pamoja maadili
ya nchi yetu kwa lengo la kuwajenga vijana wawe wanamcha mungu hasa kipindi
hiki cha mfungo wa ramadhan” alisema Kabati
Kabati alisema kuwa ametoa sadaka ya tende tani mbili
ambayo ipo katika halmashauri ya manispaa ya Iringa kwa ajili ya misikiti yote
na vituo vya watoto yatima ambavyo vinawatoto wa kiislam ambao wanafunga katika
kipindi hiki cha mfungo.
“Mimi nimeleta tani mbili ili kuongezea nguvu wafungaji wa
kipindi hiki lakini kutoa sadaka kwa mwenyezi mungu katika kipindi ambacho
waislamu wapo kwenye mfungo wa ramadhan nakuwasidia wale ambao hawana uwezo wa
kununua tunda hili la tende” alisema Kabati
Kwa upande wake mgeni rasmi Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina
Masenza amemshukuru mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringakupitia chama cha
mapinduzi (CCM) Ritta Kabati kwa kutoa sadaka ya tunda la tende kwa waiislamu
katika kipindi hiki cha mfungo wa ramadhan.
“Tunashukuru sana kwa sadaka hii ambayo umetusaidia kwa
waislam wa manispaa ya Iringa kwa msaada wako ambao utasiadia kwa wale ambao
wanamahitaji maalumu na mungu atakuongezea aple ulipopunguza na mungu
akubariki” alisema Masenza
Masenza aliwaomba maimamu kuwagawia tende hizo waislam
ambao hawana uwezo wa kununua tende tukani ili nao wapate hiki chakula cha
kwanza pindi unapofungua na wale wenye uwezo wa kununua tende dukani basi
waendelee kununua
Naye mkuu wa walimu na msimamizi wa misikiti ya Dhinureyn
Tanzania Abdul Salam Ahmad Ayub alisema kuwa msaada aliotoa mbunge wa viti
maalum mkoa wa Iringakupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati utawasaidia
waislam waliofunga.
“Sadaka hii aliyoitua huyu mbunge Kabati umekuja wakati
muafaka na umamanufaa makubwa sana kwa waislam kwa kuwa tumehimizwa kufuturu
kwanza tende hivyo kwa muislam kula tende ni fadhila kubwa sana”alisema Ayub
Ayub alisema kuwa katika kipindi hiki cha mfungo waislam
tunatakiwa kupeana vyakula ili kila mtu ambaye hana kitu aweze kupata chakula
na ndio alivyofanya huyu mbunge Ritta Kabati kwa waislam wa manispaa ya Iringa.
“Zamani watu walikuwa wanatandika jamvi nje wakati wa
kufutulu ili waweze kufutulu na waislam ambao hawana uwezo na ndio uzalendo
wenyewe huo,hivyo tunamuombea mbunge huyu aendelee na moyo huo huo” alisema
Ayub
No comments:
Post a Comment