Friday, December 1, 2017

RUNZEWE ACADEMY FC YAJINYAKULIA USHINDI KWA MARA YA PILI KWENYE MICHUANO YA DOTO CUP 2017

Kombe la mashindano ya Doto Cup likiwa mezani kabla ya kumpata mshindi.

Mchezo wa pikipiki pia ulihusika katika kusindikiza michuano ya Doto Cup.

Vikosi vya Karate vikiwa uwanjani kwenye ushiriki wa Bonanza la Doto Cup 2017.

Mgeni Rasmi ambaye ni Katibu mkuu wa baraza la michezo Tanzania (BMT) Mohamed Kiganja akiwasili kwenye viwanja vya shule ya sekondari ushirombo  ambapo ndipo michuano ya Doto cup ilikuwa ikifanyika,na kushoto Mbunge wa jimbo la Bukombe Doto Biteko akimpokea mgeni rasmi. 

Mbunge wa Bukombe,Doto Biteko akiteta jambo na Katibu mkuu wa baraza la michezo Tanzania (BMT) Mohamed Kiganja wakati wa michuano ya Doto Cup. 

Vikosi vya wakimbia kwenye magunia wamama vikiwa uwanjani kwenye ushiriki wa Bonanza la Fainali Doto Cup 2017

Kikosi cha wafukuza kuku wakifukuza kuku wakati wa michuano ya Doto Cup 2017.

Mashabiki na wanachama wa Simba na Yanga wanawake wakipimana nguvu  uwanjani kwenye ushiriki wa Bonanza la Doto Cup 2017.

Meza kuu ikiongozwa na Mgeni Rasmi ambaye ni Katibu mkuu wa baraza la michezo Tanzania (BMT) Mohamed Kiganja

Mashabiki na wanachama wa Simba na Yanga wanaume wakipimana nguvu  uwanjani kwenye ushiriki wa Bonanza la Doto Cup 2017




 Timu ya Runzewe Academy Fc katika Picha ya Pamoja kabla ya mchezo kuanza wa Fainali ili kumpata mshindi  wa  Ligi ya Doto Cup 2017.

 Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Mohamed Kiganja,Mhe. Doto Mashaka Biteko(Mb),Mwenyekiti wa CCM(W) Daniel Machongo na Mkuu wa Wilaya ya Bukombe wakiwa na kwenye picha ya pamoja na waamuzi wa michuano ya Doto cup 2017.
Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Mohamed Kiganja,Mhe. Doto Mashaka Biteko(Mb),Mwenyekiti wa CCM(W) Daniel Machongo na Mkuu wa Wilaya ya Bukombe wakiwa na wachezaji wa Timu ya Chui Fc kutoka Bugerenga katika Picha ya Pamoja kabla ya mchezo kuanza wa Fainali ili kumpata mshindi  wa  Ligi ya Doto Cup 2017.







(Picha na Consolata Evarist.)



Mashindano ya  Doto cup 2017 yamemalizika huku timu ya Runzewe Academy ikiibuka na ushindi wa matuta zidi ya timu ya Chui FC.

Michuano hiyo ambayo inaandaliwa na Mbunge wa jimbo la  Bukombe mkoani Geita  Doto  Biteko  kwa lengo la kuibua vipaji husuani kwa vijana yalianza kutimua vumbi mwezi wa tisa huku timu 45 zikishiriki kwenye mashindano hayo.  

Akizungumza na mtandao wa maduka online ,Kocha wa Runzewe academy Ramadhani Mgoi alisema kuwa huu ni msimu wa pili wa mashindano hayo na kwamba wao ni mala ya pili wanachukua Kombe hilo  na kwamba njia ambazo wanatumia kupata ushindi ni kujituma kwenye mazoezi na wachezaji kuwa na nidhamu.

Hata hivyo Kocha Mgoi ameobgeza kwa kumshukuru Mbunge kwa kuendelea kuwa karibu na vijana na kuibua vipaji kwenye Wilaya hiyo.

Katibu mkuu wa baraza la michezo Tanzania (BMT) Mohamed Kiganja ambaye alikuwa mgeni rasimi kwenye fainali hizo   amehaidi mwakani kufanya   mabadiliko ya mashindano hayo ikiwa ni pamoja na  kuleta wataalamu ili wawachague wachezaji kuchezea timu ya Taifa.

“ Ili mashindano haya yaweze kufanikiwa nilazima wapunguze umri wa wachezaji kutoka miaka 15 mpaka 17 na pia natoa wito kwa halmashauri zote zilizopo nchini kutenga maeneo ya  michezo kwasababu michezo  ni ajila hivyo tukiwa na viwanja vingi kwanza vitasaidia mapato kwenye halmashauri husika”Alisema Kiganja.

Kwa upande wake Mwandaaji wa michuano hiyo ,Mh Doto Biteko alisema kuwa matarajio ni kuona vijana wa Wilaya ya Bukombe wanatoka kwenye michezo na kufika nafasi ya juu zaidi ikiwa ni pamoja na kutoa timu ambayo itapanda daraja na kuchenza fainali kubwa zinazoendelea hapa Nchini.

Imeandaliwa na Mtandao wa Maduka Online.

No comments:

Post a Comment