Friday, December 1, 2017

MHE MGAYA AGAWA VIFAA VYA MICHEZO KWA TIMU 10 MKOANI NJOMBE

Mbunge wa Viti Maalum CCM Mkoa wa Njombe NEEMA MGAYA (Kushoto) akimkabidhi Jozi ya Jezi Kepteni wa timu ya wanawake ya Mapinduzi Quuen ambao ni washindi wa michuano ya Soka la wanawake mkoani humo, Tukio ambalo limeendana na ugawaji wa vyerehani kwa wanawake wa wilaya ya Ludewa  ikiwa ni mpango wake wa kugawa vyerehani 370 kwa akinamama na vitabu vya ziada kwa Shule za Sekondari 105 za Mkoa huo.
Mbunge wa Viti Maalum CCM Mkoa wa Njombe NEEMA MGAYA (Kushoto) akimkabidhi Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Ludewa MATERNUS NDUMBARO baadhi ya vitabu vya ziada ambavyo ametoa na kufanya idadi ya Shule zote za Sekondari za umma na mbili za kidini ambazo zimepatiwa vitabu hivyo katika Wilaya za Wanging’ombe, Makete, Njombe na Ludewa mkoani Njombe kufikia 105.Wanaoshuhudia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Josephat Kandege na Katibu wa CCM Wilaya ya Ludewa.

No comments:

Post a Comment