Saturday, December 2, 2017

PSPF YATOA MIFUKO 500 YA SARUJI UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA ILEMELA

Mfuko wa hifadhi ya Jamii wa PSPF umetoa jumla ya mifuko 500 ya Saruji kwa halmashauri ya manispaa ya Ilemela ikiwa ni mchango wake katika kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Mhe Dkt John Magufuli ya kuboresha na kuimarisha elimu nchini sambamba na ufanikishaji wa Sera ya Elimu bure

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa manispaa Ilemela mara baada ya kupokea msaada huo Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula mbali na kuishukuru PSPF amewataka wadau wengine kujitokeza na kuunga mkono jitihada hizo  kuhakikisha watoto wanaosoma shule za manispaa hiyo wanapata elimu bora na katika mazingira mazuri

‘… Kwakweli tunawashukuru wenzetu wa mfuko wa hifadhi ya Jamii wa PSPF kwa msaada wao huu waliotupatia leo ila nitoe rai kwa wadau wengine wa maendeleo kutuunga mkono katika kuhakikisha tunaboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia ili watoto wetu wapate elimu bora na katika mazingira mazuri …’ Alisema

Kwa upande wake Mkurugenzi wa manispaa ya Ilemela John Wanga amesema kuwa mifuko hiyo 500 ya Saruji itaenda kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za Sekondari za manispaa yake , Vyumba vya maabara na Nyumba za walimu  kwa kadri itakavyowezekana huku akizidi kuomba ushirikiano katika kuhakikisha kwa pamoja wanafanikisha utekelezaji wa shughuli za maendeleo

Aklihitimisha muwakilishi wa PSPF amesema kuwa PSPF itaendelea kusaidia Jamii katika uboreshaji na uanzishwaji wa miradi mbalimbali kuhakikisha Jamii inapata huduma muhimu kwa wepesi na haraka kunakozingatia ubora

‘ Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga’

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
02.12.2017

No comments:

Post a Comment