Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akikagua Maghala ya Mamlaka ya Taifa ya Hifadhi ya Chakula Kanda ya Songea (NFRA) wakati wa ziara ya kikazi Wilayani Songea Mkoa wa Ruvuma, Wengine Pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Songea Mhe Pololet Kamando Mgema (Kushoto) Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu Wa (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba (Katikati) na Meneja NFRA Kanda ya Songea Ndg Amos Mtafya, Jana Novemba 2, 2017. Picha Zote Na Mathias Canal
Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisalimiana na kina mama waliojipatia kibara kwenye ujenzi wa Kituo cha mafunzo ya kilimo OTC Lilambo kitakachojihusisha na uchakataji wa mahindi kilichopo Mtaa wa Namanditi, Kata ya Lilambo, Wilaya ya Songea wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja Mkoani Ruvuma, Jana Novemba 2, 2017.
Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa (Wa tatu Kushoto) akitembelea na kukagua Maghala ya Mamlaka ya Taifa ya Hifadhi ya Chakula Kanda ya Songea (NFRA) wakati wa ziara ya kikazi Mkoani Ruvuma, Wengine Pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Songea Mhe (Kushoto) Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu Wa (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba (Wa Pili kulia) na Meneja NFRA Kanda ya Songea, Jana Novemba 2, 2017.
Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa alipotembelea Kijiini Likuyu Fusi, Kata ya Lilambo, Wilaya ya Songea Mjane Bi Ester Gama ambaye ni mke wa Marehemu Leonidas Gama akimvisha kitenge ikiwa ni ishara ya upendo na faraja. Gama alifariki Dunia Novemba 23, 2017 katika Hospitali ya Mtakifu Joseph ya Peramiho.
Jana Novemba 2, 2017.
Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua mahindi ili kubaini alipotembelea Maghala ya Mamlaka ya Taifa ya Hifadhi ya Chakula Kanda ya Songea (NFRA) wakati wa ziara ya kikazi Wilayani Songea Mkoa wa Ruvuma, Jana Novemba 2, 2017.
Naibu Waziri Wa Wizara ya
Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akikagua Maghala ya Mamlaka
ya Taifa ya Hifadhi ya Chakula Kanda ya Songea (NFRA) wakati wa ziara ya kikazi
Wilayani Songea Mkoa wa Ruvuma, Jana Novemba 2, 2017.
Na Mathias Canal, Ruvuma
Uongozi Wa Mkoa Wa Ruvuma leo Disemba 1, 2017 umeelekezwa
kuwahamasisha wakulima kujiunga na vyama vya msingi vya ushirika kwani kupitia
vikundi ndio njia muhimu na mkombozi kwa manufaa ya mkulima mmoja mmoja na
Taifa kwa ujumla.
Amebainisha hayo Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary
Mwanjelwa wakati akizungumza na baadhi ya wakulima sambamba na viongozi Wa
wakulima katika Mkutano Wa hadhara ulifanyika katika eneo la Ofisi za Wakala wa
Taifa wa Hifadhi ya Chakula Kanda ya Songea.
Pamoja na kuwasisitiza wakulima hao kujiunga katika vikundi vya
vyama vya msingi vya ushirika, Mhe Naibu Waziri ameelekeza uongozi Wa Mkoa Wa
Ruvuma kutilia msisitizo umuhimu Wa Vyama hivyo kwani ni maelekezo ya ilani ya
Ushindi ya Chama Cha Mapinduzi katika kipindi cha miaka mitano 2015-2020
inayotekelezwa na serikali ya awamu ya Tano ikiongozwa na Mhe Rais Wa Jamhuri
ya Muungano Wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.
Alisema kuwa vikundi hivyo vikianzishwa na kuwa na Uongozi
vitarahisisha kuuza mazao mazuri kwani kutakuwa na nguvu ya pamoja
inayowakutanisha kwa kuongozwa na sheria na taratibu walizojiwekea kama kikundi
pasina kuwa kinyume na taratibu za serikali.
"Upo umuhimu mkubwa Wa kujiunga na AMCOS kwani ni jambo
lisilokuwa la hiari ambapo itarahisisha kupata mikopo huku kwa serikali ikiwa
ni njia rahisi kuwahudumia, Aidha Elimu inapaswa kutolewa juu ya umuhimu Wa
Vyama vya msingi vya ushirika" Alikaririwa Mhe Mwanjelwa
Aliongeza kuwa Mamlaka ya Taifa ya Hifadhi ya Chakula nchini
inapaswa pia kutoa Elimu kwa umma juu ya majukumu yake kwamba ni kununua
mahindi na kuyahifadhi ili kuwa na akiba pindi panapotokea Ukame serikali iweze
kuwahudumia.
Awali Naibu Waziri Wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa alitembekea na
kukagua Ghala La kuhifadhi mahindi Kanda ya Songea ambapo ameshuhudia akiba ya
kutosha ya mahindi ambapo mpaka kufikia Leo Disemba 2, 2017 Kanda ya Songea ina
mahindi yanayofikia Tani 21,892.924 huku kati yake Tani 10,335.395 ni ununuzi
Wa msimu Wa mwaka 2016/2017 na Tani 11,557.529 ni ununuzi Wa mwaka huu 2017/2018.
Aidha, Mhe Mwanjelwa amezuru Kijiini Likuyu Fusi, Kata ya
Lilambo, Wilaya ya Songea na kutoa pole kwa Ndugu na Jamaa akiwemo Bi Ester
Gama ambaye ni mke Wa aliyekuwa Mbunge na Diwani wa Songea Mjini Mkoani Ruvuma,
Marehemu Leonidas Gama aliyefariki Dunia Novemba 23, 2017 Majira ya saa 4:25
Usiku katika Hospitali ya Mtakifu Joseph ya Peramiho iliyopo Songea baada ya
kukimbizwa huko kwa matibabu baada ya kuugua ghafla.
MWISHO
No comments:
Post a Comment