Tuesday, November 14, 2017

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji akutana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage amekutana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa alieambatana na wawekezaji wa Kichina walioonesha nia ya kuwekeza katika mkoa wa Iringa.
 

katika Ziara hiyo, Mkuu wa mkoa wa Iringa Mhe Bi. Amina Masenza ameelezea mikakati iliyopo katika mkoa wake ya kuhakikisha anapokea wawekezaji na kuwapatia maeneo ya kujenga Viwanda ili kuhahakisha wananchi wanaajiriwa kukuza kipato chao.

Mhe. Waziri amesifu jitihada zinazofanywa na Viongozi wa Mkoa wa Iringa katika kuhakikisha wanahimiza ujenzi wa Viwanda na kushirikiana na wawekezaji.

 
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage (Mb) akimsikiliza kwa makini mkuu wa mkoa wa Iringa Mhe. Bi, Anna Masenza.
Wawekezaji walioonesha nia ya ya kuwekeza katika Mkoa wa Iringa, wakisikiliza kwa makini majadiliano yakiendelea katika ofisi ya Mhe. Waziri wa Viwanda.
Wajumbe kutoka Mkoa wa Iringa wakimsikiliza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji wakati wakujadili masuala mbalimbali ya uwekezaji katika mkoa wa Iringa.

No comments:

Post a Comment