Wakati Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam *Mhe Paul Makonda* akiwakarabisha Kundi la Madaktari
Bingwa ambao ni Askari wa Kikosi cha Maji kutoka Jeshi la Jamhuri ya
watu wa *China* nchini *Tanzania* ambao watakuja Tanzania na Meli kubwa
ya Kikosi cha Wanamaji kutoka Jamhuri ya watu wa China wakiwa zaidi ya
Wanajeshi na Madaktari *380* ikiwa ni Utekelezaji wa Kauli ya *Balozi wa
China* aliemaliza muda wake nchini, ambapo alimhakikishia Mhe Makonda
kuleta Timu ya Madaktari Bingwa watakaokuja kumsaidia katika juhudi zake
za kutoa Huduma bora za Afya kwa Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam
wasiokuwa na kipato *KIKUBWA* cha kumudu gharama za matibabu.
Kutokana na Uwepo wa
Madaktari Hao, *Mhe Makonda* ametangaza tena Kuanza kwa Zoezi jingine la
kutoa Matibabu Bure, pamoja na vipimo *BURE* kwa Wananchi wa Mkoa wa
Dar es Salaam Kuanzia Tarehe 19 mpaka 25 mwezi huu (19-25/11/2017)
matibabu ambayo yatatolewa Ndani ya Meli ya Kichina itakayoweka Nanga
katika Bandari ya Dar es Salaam.
Pamoja na kutoa
Matibabu Meli hiyo pia itatoa Huduma za upasuaji mdogo na mkubwa pamoja
na kutoa dawa kwa watakaobainika kuitaji dawa, watakuja na baadhi ya
vifaa vya kusaidia kutengeneza Mashine zetu za x Ray na vipimo vingine
ambazo ni mbovu katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Mhe Makonda amewataka wananchi kujitokeza kwa winging katika kuchangamkia *FURSA* ya Matibabu Bure kutoka China.
Katika hatua za awali
za Utoaji wa matibabu Bure baadhi ya Watu wasiokuwa na Nia njema
WALIBEZA jitihada za Makonda za Utoaji wa Huduma za Matibabu na upimaji
*BURE* , lakini sasa Dunia imetambua na kuamua kumuunga mkono katika
Juhudi zake za kuhakikisha wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam wanapata
huduma bora za Afya kwa *Gharama nafuu*
No comments:
Post a Comment