Sunday, November 12, 2017

Watumishi Wa Wizara Ya Maliasili Na Utalii Wahimizwa Kutoa Ushirikiano ili Kukuza Utalii




Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakiwa kwenye picha ya pamoja mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam  na aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya  Maendeleo ya Utalii katika Idara ya Utalii, Bi. Uzeeli Kiangi (katikati)  katika hafla fupi ya kumuaga baada ya kustaafu mapema mwezi Julai mwaka huu kwa mujibu wa Sheria ya utumishi wa Umma. Kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara Utalii, Bw. Deograsius Mdamu na Afisa Utalii Domina Moshi (kushoto) ( Picha na Lusungu Helela- MNRT)


Aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya  Maendeleo ya Utalii katika Idara ya Utalii, Bi. Uzeeli Kiangi akizungumza jijini Dar es Salaam  na Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii  katika hafla fupi ya kuagwa kwake baada ya kustaafu mapema mwezi Julai mwaka huu kwa mujibu wa Sheria ya utumishi wa Umma. Kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara Utalii, Bw. Deograsius Mdamu.


Kaimu Mkurugenzi wa Idara Utalii, Bw. Deograsius Mdamu (kushoto) akimkabidhi moja ya  zawadi ya saa ya mezani yenye picha ya aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya  Maendeleo ya Utalii katika Idara ya Utalii, Bi. Uzeeli Kiangi katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ya kumuaga baada ya kustaafu mapema mwezi Julai mwaka huu kwa mujibu wa Sheria ya utumishi wa Umma 


Aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya  Maendeleo ya Utalii katika Idara ya Utalii, Bi. Uzeeli Kiangi akiwa na Afisa Utalii, Nina Kisando (katikati) wakiwa wanatabasamu huku  wakionesha moja ya zawadi ya saa ya mezani yenye picha ya Bi. Kiangi aliyokabidhiwa katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki  baada ya kustaafu mapema mwezi Julai mwaka huu kwa mujibu wa Sheria ya utumishi wa Umma. Kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Bw. Deograsius Mdamu.


Baadhi ya Watumishi wa Idara ya Utalii wakimsikiliza aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya  Maendeleo ya Utalii katika Idara ya Utalii, Bi. Uzeeli Kiangi akizungumza katika hafla ya kustaafu kwake kwa Mujibu wa Sheria ya  Utumishi wa Umma.


Aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya  Maendeleo ya Utalii katika Idara ya Utalii, Bi. Uzeeli Kiangi akikata keki katika katika hafla ya kustaafu kwake kwa Mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma tayari kuwalisha Watumishi wa Wizara. Kushoto kwake ni Marygoreth Mushin a Kulia kwake ni Mary Msekela.


Aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya  Maendeleo ya Utalii katika Idara ya Utalii, Bi. Uzeeli Kiangi akimlisha keki Afisa Utalii Mwandamizi ikiwa ni ishara ya kuagana katika hafla ya kustaafu kwake kwa Mujibu wa  Sheria ya Utumishi wa Umma. Kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Bw. Deograsius Mdamu.


Aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya  Maendeleo ya Utalii katika Idara ya Utalii, Bi. Uzeeli Kiangi ( wa pili kushoto) akisindikizwa na baadhi ya Watumishi wa Idara ya Utalii mara baada ya hafla ya kustaafu kwake kwa Mujibu wa  Sheria ya Utumishi wa Umma.


Aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya  Maendeleo ya Utalii katika Idara ya Utalii, Bi. Uzeeli Kiangi ( wa pili kushoto) akiwa na Afisa Utalii, Dorothy Mtweve mara baada ya hafla ya kustaafu kwake kwa Mujibu wa  Sheria ya Utumishi wa Umma kumalizika.
 

Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii katika Idara ya Utalii wameombwa kumpa ushirikiano Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii Deograsius Mdamu, ili aweze kutimiza majukumu yake kwa ufanisi

Kauli hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki katika ofisi ndogo ya Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Dar es Salaam  na aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi   Sehemu ya Maendeleo  ya Utalii katika Wizara hiyo , Bi. Uzeeli Kiangi  katika hafla fupi iliyoandaliwa kwa ajili ya kumuaga baada ya kustaafu mwanzoni mwa mwezi Julai kwa mujibu wa Sheria ya utumishi wa Umma akiwa ameitumikia Wizara kwa kushika nafasi mbalimbali kwa muda wa miaka 33.

Akizungumza katika hafla hiyo alisema  ‘’ Watumishi ni kiungo muhimu katika kumsaidia Mkurugenzi wa Idara ya Utalii kutekeleza majukumu yake, ni matumaini yangu kuwa mtampa ushirikiano katika hili’’

Amesema kupitia  ushirikiano huo  utasaidia kupelekea Wizara kutimiza azma ya kufikia watalii milioni 8 na fedha za kigeni dola bilioni 20 kila mwaka kufikia mwaka 2025

Aidha, Bi.Kiangi aliwataka watumishi kuzingatia miiko ya kazi zao kwa kutojihusisha na vitendo vya kupokea rushwa wanapotimiza majukumu yao, la sivyo serikali hii ya awamu ya tano haitawaacha salama.

‘’Wakati wa utumishi wangu nilijitahidi kukwepa kupokea rushwa kwa kuwa sikujua huyu anayetaka kunihonga katumwa na nani na kwanini anipe rushwa wakati natimiza majukumu yangu jihadharini na watoa rushwa’’ alisisitiza

Katika hatua nyingine,  Bi. Kiangi aliwataka  watumishi wenye tabia ya kujituma kufanya kazi pale tu wanapohisi kazi hiyo ina malipo wajirekebishe mara moja kwa kuanza kufanya kazi zote zenye malipo na zisizo na malipo kwani zina umuhimu katika kuwajenga kitaaluma.

Awali, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Deograsius Mdamu alisema Idara yake imejipanga kufanya kazi kwa kasi zaidi na kuendeleza yale ambayo Mkurugenzi Msaidizi, Bi. Kiangi aliyokuwa akiyapigania kwa ajili ya maendeleo ya utalii.

‘’Wizara inatambua mchango wako tangu ulipoajiriwa mwaka 1984, tunakuahidi tutakutumia pale tunapohitaji utaalamu wako ili kuhakikisha Wizara inafikia malengo iliyojiwekea’’ alisisitiza

Kwa upande wake, Afisa Utalii Mwandamizi, Josephat Msimbano  wakati  amesema Bi. Uzeeli Kiangi wakati wa utumishi wake alikuwa ni kiongozi aliyeichukia rushwa na yeyote aliyethubutu kutaka kumhonga ili ahudumiwe kwa minajili ya kupindishwa kwa sheria  aligonga mwamba.

Naye Afisa Utalii, Domina Moshi  amesema kwa upande wake, Bi Uzeeli Kiangi alikuwa ni mshauri mzuri, alikua zaidi ya mama na alipenda watumishi wajiendeleze kielimu na ndiye aliyemfanya aende masomoni nchini kujiendeleza kielimu.

Bi. Uzeeli Kiangi kastaafu kwa Mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma akiwa ameihudumia Idara ya Utalii katika nafasi mbalimbali kwa muda wa miaka 33 ambapo aliajiriwa mwaka 1984 kama Afisa Utalii Daraja la tatu ambapo alipandishwa madaraja hadi kufikia Afisa Utalii Mwandamizi daraja la kwanza mwaka 2007.

Mwaka huo huo alipandishwa kuwa Mkurugenzi Msaidizi kusimamia Sehemu ya Leseni na Uthibiti kwa kipindi cha miaka mitano. Pia, mwaka 2013 hadi julai 2017 alikuwa Mkurugenzi Msaidizi kusimamia Sehemu ya Maendeleo ya Utalii

No comments:

Post a Comment