Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim
Wangabo amesifu kikundi cha kinamama wanaojishughulisha na kazi za
ujenzi katika Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi alipotemnbelea maendeleo ya
ujenzi wa kituo cha afya Nkomolo wilayani humo.
Amesema kuwa serikali itaendelea
kutoa ajira kwa vikundi mbalimnbali kwa makundi yote ya wananwake na
vijana wanaojishughulisha na ujenzi kutokana na kuwa na miradi mingi
inayohitaji ujuzi wao na kuwaasa wanawake na vijana waige mfano huo ili
waweze kujiwezesha kuliko kukaa vijiweni na kuendelea kuilaumu serikali.
“Nimependezwa na ujasiri wa hawa
kina mama amabo sikutegemea kuwaona hapa, kwa namna wanavyofanya kazi
nimefarijika sana, itabidi na wanawake wengine wanaokaa majumbani waige
mfano wao kuliko kukaa tu na kusubiri kuletewa,” Alibainisha.
Ujenzi huo unaofanywa kwa mradi
wa kuboresha vituo vya afya 172 nchini kwa fedha zilizotolewa na Wizara
ya OR – TAMISEMI zilizochangwa na wadau wa maendeleo duniani wakiwemo
benki ya dunia na wengineo.
Kwa upande wake mmoja wa wanawake
hao Salome Sululu amethibitisha kuwa wamekuwa wakifaidika kwa kibarua
hicho walichokipata na fedha wanazopatiwa kuwa zinawasaidia kujikimu
katika familia na kuwawezesha kupata mitaji ya kujiendeleza kwenye
kilimo na kusifu utaratibu wa serikali wa kuajiri vibarua wa maeneo
husika bila ubaguzi.
No comments:
Post a Comment