Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mwanza umemaliza salama uchaguzi wa kupata viongozi wapya kwa awamu ya 2017-2022 kwa nafasi mbalimbali za Uongozi
Akizungumza katika mkutano huo mwenyekiti wa muda wa Uchaguzi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilemela Comred Dkt Angeline Mabula mbali na kuwashukuru wakina mama hao kwa kumuamini na kumchagua kuwa mwenyekiti wa muda wa uchaguzi amewatakia heri wagombea wote waliochaguliwa huku akiwaasa kuwatumikia vyema wanachama waliowaamini na kuwachagua
‘… Nawashukuru sana wakina mama kwa kuniamini na kunichagua kuwa mwenyekiti wa muda wa uchaguzi huu nawashukuru kwa heshima mlionipa na kazi niliyopewa imekwisha salama na tuwatakie heri wale waliochaguliwa wote kwa nafasi mbalimbali walizoomba …’ Alisema
Akitaja matokeo ya uchaguzi huo msimamizi wa uchaguzi na mjumbe wa kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mwanza Comred John Mongela amemtangaza Bi Ellen Bogohe kuwa Mwenyekiti mpya wa Umoja huo wa kina mama wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mwanza kwa kupata kura 268 huku mpinzani wake Bi Frola Magabe akimfuatia kwa Kura 196 wakati nafasi ya Ujumbe wa Baraza kuu la UWT Taifa ikienda kwa Comred Dkt Angeline William Samike kwa kuwatangulia wenzake kwa kura 267 huku nafasi za uwakilishi kutoka UWT kwenda VIJANA na kutoka UWT kwenda WAZAZI zikirudiwa kwa mara ya pili baada ya wagombea kushindwa kufikisha nusu ya kura zote
Akihitimisha Mwenyekiti wa Umoja huo wa kinamama UWT aliyechaguliwa leo Bi Ellen Bogohe amewashukuru wajumbe wa mkutano huo na wasimamizi wa uchaguzi kwa kumuamini kwa mara ya pili na kutenda haki huku akiwataka kuweka pembeni tofauti zao za kipindi cha Uchaguzi na kuungana tena kwa maslahi ya Jumuiya yao na Chama
‘ Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga ’
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
28.11.2017
No comments:
Post a Comment