Vijana wa UVCCM wakisimika bendera ya chama cha mapinduzi. |
Katibu wa UVCCM Wilayani Geita pamoja na vijana wakikimbia wakati wa zoezi la kuweka bendera. |
Vijana wa UVCCM wakisimika bendera ya chama cha mapinduzi. |
Katibu wa UVCCM,Ally Rajabu akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa chama pamoja na mabarozi wa mashina. |
PICHA NA JOEL MADUKA
Vijana hamsini (50 )wa chama cha demokrasia na
maendeleo( CHADEMA )wamekihama chama hicho na kujiunga na chama cha mapinduzi(
CCM) katika kijiji cha Buligi kata ya Senga wilayani Geita wakati wa uzinduzi
wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani katika Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa
chama hicho, (UVCCM).
Akizungumza
kwenye uzinduzi huo ulioambatana na zoezi la kusimika bendera kwamabalozi,
Katibu wa UVCCM wilayani Geita Bw Ali Rajab alisema vijana hao wamehama Chadema na kujiunga na CCM
kutokana na kasi ya utendaji ya Rais Dr John Magufuli.
Bw Rajab pia
amewataka pia ameongeza kwa kuwataka watumishi kuacha kufanya kazi kwa mazoea ili
kuendana na kasi ya Rais Magufuli na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa ujumla.
Katibu wa
Jumuiya ya Umoja wa wanawake, UWT wilayani Geita Bi Mazoea Salim, amesema
wanatarajia kushinda kwenye uchaguzi huo mdogo katika kata ya Senga .
No comments:
Post a Comment