Taasisi ya The Angeline Foundation iliyoasisiwa na Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula kwa lengo la kusaidia utatuzi wa changamoto zinazowakabili wananchi wa Jimbo la Ilemela imefanikiwa kuwapatia ufadhili wa matibabu wagonjwa watatu kutoka Jimbo la Ilemela akiwemo Yohana Makoye kutoka kata ya Sangabuye, Hussein Nassoro wa kata ya Nyasaka na Omary Mayunga kutoka Ngh’ungumarwa
Akizunguza mara baada ya kuwatembelea wagonjwa hao katika hospitali ya CCBRT ya Jijini Dar es Salaam Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula amesema kuwa wagonjwa hao walikuwa wakisumbuliwa na matatizo mbalimbali mfano wa Yohana aliyejeruhiwa na Fisi miaka mitatu iliyopita na kukosa matibabu sahihi huku akiishukuru Taasisi ya Nitetee Foundation iliyoshirikiana na Taasisi yake kupata ufadhili kutoka kwa The Desk Chair Foundation ya Mkoa Mwanza iliyokubali kugharamia matibabu hayo
‘… Taasisi ya The Angeline Foundation itaendelea kushirikiana na taasisi nyengine kuhakikisha tunamaliza kama si kupunguza changamoto zinazowakabili wananchi wa Jimbo la Ilemela na tumeanza muda mrefu kufanya hivyo ipo miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na The Angeline Foundation na ipo mipango mbalimbali inakuja kwaajili wa wananchi wa Jimbo langu kikubwa ni kuendelea kutoa ushirikiano …’ Alisema
Aidha Mhe Dkt Angeline Mabula amewahakikishia wananchi wa Jimbo la Ilemela kuendelea kupamba na katika kuhakikisha wanayafikia malengo ya Serikali ya awamu ya Tano chini ya Mhe Rais Dkt John Magufuli sanjari na kuwasisitiza kuunga mkono na kutoa ushirikiano katika kuyafikia malengo hayo
Kwa upande wao wagonjwa waliopata ufadhili huo wamemshukuru Mhe Dkt Angeline Mabula kupitia Taasisi zilizoshirikiana kufanikisha matibabu hayo huku wakitoa wito wa kumuunga mkono kiongozi huyo kuhakikisha wnanchi wa Ilemela wananufaika
‘ Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga’
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
06.11.2017
No comments:
Post a Comment