Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Ajira na Watu wenye ulemavu
Jenista Mhagama,akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa
Mkoa wa Geita na wabunge wa majimbo yaliyopo Mkoani humo.
(Na Joel Maduka. )
Mbunge wa Jimbo la
Bukombe Doto Mashaka Biteko,amewaomba wananchi ambao wamepatiwa mikopo kutoka baraza la utendaji la uwezeshaji wananchi
kiuchumi kutumia fedha hizo kwa manufaa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha
wanainuka kiuchumi kutoka hapo walipo kwenda juu zaidi.
Rai hiyo ameitoa
wakati wa shughuli za kukabidhi hundi kwa wajasiriamali 3824 ambao
wanajumuhisha mikoa mine ya kanda ya ziwa.
Mheshiwa Doto,alisema
kuwa ni vyema Mikopo ambayo wamepatiwa ikageuka kuwa nuru kwenye maisha yao na
sio kuleta shida hali ambayo inaweza kupelekea wakaanza kukimbia hata pindi wanapoona
magari ya viongozi wa serikali wakiwemo wakuu wa Wilaya.
“Kwa wale ambao
watapokea mikopo hii leo(jana) wapo pia wananchi wa wilaya ya Bukombe
nimeambiwa kuwa jumla wapo 422 kati yao 322 ni wakina mama kwa hiyo
utaona zaidi wakinamama wamepata fursa hii na mimi niseme tu mheshimiwa waziri
sisi wananchi wa Bukombe tunakushukuru sana lakini niwaomba wananchi
tusikimbiane baada ya kuwa tumekopa hisiwe kukopa furaa kulipa ni majanga”Alisema
Doto.
Doto aliendelea
kuwaomba wananchi hao baada ya mwaka wanapokutana basi kila mmoja awe anajambo
ambalo amelipata kutokana na kupatiwa mikopo hiyo.
Aidha kwa upande
Mwingine Doto amemshukuru Mheshimiwa, Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana,
Ajira na Walemavu Jenista Mhagama kwa kuendelea kutenda kila jambo ambalo
amekuwa akilisema.
Naye Mbunge wa Nyang'hwale Hussen Kasu ametumia nafasi hiyo kuziomba taasisi za mikopo kuelekeza nguvu za
mikopo kwenye jimbo lake kwani pia kuna watu ambao wanauitaji wa kukopa.
Hata hivyo kwa upande
wake , Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama amewasisitiza wananchi kuchangamkia fursa ya
mikopo kwani hayupo mtu ambaye ameendelea bila ya kukopa hivyo ni vyema
wakatumia njia hizo kama sehemu ya kujikwamua na kujiinua kiuchumi.
Vikundi vya Wajasiriamali
waliofaidika ni kutoka Mkoa ya Kagera,Geita,Simiyu,Mara na Mwanza na jumla ya
wajasiriamali 3824 kati yao wanawake ni 2,161 sawa na asilimia 57.Jumla ya
Mikopo iliyotolewa kwa Wajasiriamali ni zaidi ya Bilioni mbili.
|
No comments:
Post a Comment