Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira)
Mh. Anthony Mavunde leo ametembelea Chuo cha Ufundi Don Bosco kilichopo mkoani
Kilimanjaro na kukagua maendeleo ya Vijana ambao wanasomeshwa hapo na Serikali
kupitia mpango wa Ukuzaji Ujuzi Nchini.
Akizungumza na Vijana hao ambao wanasomea masomo ya Komputa,Mavunde
amewataka Vijana hao kuutumia ujuzi watakaoupata hapo chuoni kujiajiri
kwa kuunda vikundi na Makampuni ili wapate nafasi ya kuwezeshwa kupitia
mifuko ya uwezeshwaji wananchi kiuchumi nchini na hivyo kusaidia kutatua
changamoto ya ukosefu wa Ajira kwa Vijana.
Mavunde pia amewaeleza Vijana hao kwamba watambue siku zote wao
ndio moyo wa Taifa na hivyo ndio nguvu
kazi inayotegemewa kwa kiasi kikubwa ndio maana Serikali inaona umuhimu wa
kuwekeza katika Mpango huu wa ukuzaji Ujuzi ili kuhakikisha Taifa linakuwa na
nguvu kazi yenye ujuzi stahiki katika kuelekea nchi Uchumi wa Viwanda na ya
kipato cha kati.
Kwa upande wao Vijana hao wanufaika na Mpango huu wameishukuru
serikali kwa kutekeleza mpango huu wa ukuzaji ujuzi ambao utawasaidia kupata
ujuzi na baadaye kuweza kujiajiri na Kuajiri Vijana wengine.
No comments:
Post a Comment