Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selamani Jafo akifungua
kongamano ya Chama cha Wahasibu Tanzania linalofanyika Mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Wahasibu
Tanzania Fred Msemwa akitoa neno la utangulizi wakati wa ufunguzi wa
Kongamano linalohusu uwazi na uwajibikaji kwa viongozi wa Mamlaka za
Serikali za Mitaa.
Washiriki na wajumbe wa chama cha
Wahasibu Tanzania wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya Ufunguzi wa Kongamano
lililofunguliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za MItaa Mhe.Selemani Jafo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(kulia)
akizungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Wahasibu Tanzania Fred Msemwa
wakati wa Ufunguzi wa Kongamano linalofanyika Mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(Katikati mbele)
akiwa katika Picha ya pamoja na viongozi wa chama cha wahasaibu Tanzania
pamoja na wawwezeshaji wa Kongamano hilo.
……………..
Nteghenjwa Hosseah,OR-TAMISEMI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo amewataka
watendaji Mamlaka za Serikali za Mitaa kudhibiti matumizi yasiyo ya
lazima kwenye Halmashauri ili kufanikisha utekelezaji wa miradi ya
maendeleo.
Waziri Jafo ameyasema hayo
wakati wa Ufunguzi wa kongamano la siku mbili la Chama cha Wahasibu
Tanzania(TAA) lililojumuisha wataalam wa Hesabu na wafanya maamuzi
kutoka katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa.
Katika Kongamano hilo ambalo
Linafanyika kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa Chama hicho mwaka
1983 limelenga kujenga uwezo kuhusu Uwazi na Uwajibikaji kwa Viongozi
waandamizi wa Mamlaka ta Serikali za Mitaa katika Matumizi ya Fedha za
Umma.
Waziri Jafo amesema kuwa
Bajeti kubwa ya Serikali inapelekwa kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa
takribani asilimia 20.7 ya Bajeti ya Serikali huelekezwa katoka
Halmashauri hivyo ni eneo ambalo linapata Fedha nyingi na zinahitajo
uangalizi mkubwa.
Tunafahamu kuwa Viongozi wa
Halmashauri mna Mamlaka kamili ya kupanga matumizi ya Fedha hizo lakini
angalieni maeneo ambayo yataleta Tija kwa Wananchi na yatatatua
changamoto zinazowaathiri wananchi wetu katika maisha yao ya kila siku,
huko ndio sehemu ya kutumia Fedha nyingi na si vinginevyo.
Katika maeneo ambayo hayanipi
amani na bado nayaona kuwa na matumizi mabaya ya Fedha ni eneo la
Manunuzi ya Umma nawasihi muwaelimisha vya Kutosha viongozi hawa namna
ya kudhibiti mianya yote ya Upotevu wa Fedha uliopo katika eneo la
Manunuzi”
Alisema Jafo.
Aliongeza kuwa kuna tabia ya
kubadilisha matumizi ya vifungu”Realocation” bila sababu za Msingi na
bila kufuata taratibu zinazohitajika suala hili limekua likisababisha
hoja nyingi wakati wa Ukaguzi wa Hesabu nawasili viongozi wa Mamlaka za
Serikali za Mitaa mkaliangalie hilo kwa jicho la tati na mkalidhibiti.
Akitoa neno la Ufunguzi
Mwenyekiti wa Chama cha Wahasibu Tanzani Fred Msemwa amesema Chama hiki
kina umri wa Miaka 34 na kina lengo la kuendeleza Taaluma za Uhasibu
Tanzania na kutoa elimu ya Fedha na Biashara kwa wananchi ili waweze
kujisimamia katika mapato na matumizi yao.
Msema alisema kuwa
wamefanikiwa kutoa elimu ya Kodi, Ongezeko la Thamani,sheria za Fedha na
mabadiliko yake pamoja na kuanzisha Dawati la Mhasibu ambalo hutoa
uelewa kwa wananchi kuhusu masuala ya Fedha, biashara na Rasilimali.
Kongamano hili ni endelevu na
litakua likifanyika kila mwaka na litakuwa likiwajengewa uwezo viongozi
wa Serikali ambao wengine hawana utaalam wa Uhasibu namna ya kuipitia
kwa umakini taarifa ya Mkaguzi wa Ndani, viashiria vya Rushwa katika
matumizi ya Fedha za Umma, kuzuia vihatarishi, namna ya kuongeza vyanzo
vya mapato na namna ya kupata Fedha za Utekelezaji wa Miradi ya
Maendeleo.
No comments:
Post a Comment