Msanii Baraka The Prince amemlaumu meneja wake wa zamani chini ya
RockStar 4000 Seven Mosha pamoja na mpiga picha maarufu Mx Carter, kuwa
ndio wanaohusika na kufelisha kazi yake mpya YouTube.
Baraka ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye eNewz ya East Africa
Television, na kusema kwamba watu hao wawili ndio walikuwa na ‘access’
ya acount yake ya YouTube, hivyo wao ndio watakuwa wahusika.
Baraka ameendelea kwa kusema kwamba mara ya kwanza walimfanyia hivyo
kwenye acount yake ya zamani ambayo ilikuwa inasimamiwa na RockStar 400,
views zilikuwa zinapungua badala ya kuongezeka huku wengine
waklimlalamikia kuwa hawaioni YouTube, hivyo aliamua kuifuta na kufungua
mpya, na hata hivyo waliendelea kufanya hivyo kwa acount hiyo mpya.
Bongo Movies
No comments:
Post a Comment