Baadhi ya Makatibu wakuu kutoka
Wizara mbalimbali wakifuatilia mada iliyowasilishwa na Mkurugenzi Mkuu
wa Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) Bw.Nehemia Mchechu(hayupo pichani)
kuhusu ujenzi wa Mji mpya wa Serikali unaotarajiwa kujengwa mjini
Dodoma.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
Mha.John Kijazi akipata maelezo kuhusu ujenzi wa Mji mpya wa Serikali
unaotarajiwa kujengwa mjini Dodoma katika eneo la Ihumwa kutoka kwa
Mkurugenzi wa mipango Miji nchini Profesa John Lupala leo Mjini Dodoma.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
Mha.John Kijazi akitembelea eneo ambalo utajengwa mji wa Serikali
katika eneo la Ihumwa leo Mjini Dodoma.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
Mha.John Kijazi akionyeshwa ramani ya mpangilio wa mji wa Serikali
utakavyokuwa na Mkurugenzi wa mipango miji nchini Profesa John Lupala
wakati katibu kiongozi alipotembelea eneo hilo na makatibu wakuu leo
Mjini Dodoma.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
Mha.John Kijazi akipata maelezo mbalimbali katika eneo ambalo Serikali
inajenga mji katika eneo la ihumwa Mjini Dodoma.Katibu Mkuu Kiongozi
aliambatana na Makatibu wakuu wa Wizara mbalimbali katika ziara hiyo.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
Mha.John Kijazi akionyeshwa ramani ya mpango wa matumizi ya ardhi ya
eneo ambalo unajengwa mji wa Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Nyumba la Taifa(NHC) Bw.Nehemia Mchechu katika eneo la Ihumwa mjini
Dodoma.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
Mha.John Kijazi akiuliza swali wakati akionyeshwa ramani ya mpango wa
matumizi ya ardhi ya eneo ambalo unajengwa mji wa Serikali katika eneo
la Ihumwa Mjini Dodoma.Wanaompa maelekezo ni Mkurugenzi wa mipango miji
nchini Profesa John Lupala na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la
Taifa(NHC) Bw.Nehemia Mchechu
Picha zote na Daudi Manongi,MAELEZO,DODOMA.
……………
Frank Mvungi- Maelezo, Dodoma
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
Mhandisi John Kijazi na Makatibu Wakuu leo wametembelea na Kukagua eneo
utakapojengwa Mji wa Kisasa wa Serikali katika eneo la Ihumwa Mjini
Dodoma ili kujionea hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa mradi huo.
Akizungumza katika eneo la mradi
unaotarajiwa kutekelezwa katika eneo lenye ukubwa ekari 1500 Balozi
Kijazi amesema kuwa Mji huo utakuwa wa kipekee na hiyo ni sehemu ya
mikakati ya Serikali kuhakikisha kuwa Makao Makuu ya nchi yanakuwa
katika mpangilio wa kisasa ili kuleta tofauti kati ya mji huo na miji
mingine.
“ Niwatoe wananchi shaka kuhusu
Serikali kuhamia Dodoma kwa kuwa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano
inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli imeshaanza
kutekelezwa kwa vitendo na sehemu kubwa ya Watumishi wa Serikali
wameshahamia hapa Dodoma Wakiwemo Mawaziri na Makatibu Wakuu” .
Alisisitiza Balozi Kijazi
Akifafanua amesema kuwa mji huo
utakuwa na maeneo kwa ajili ya majengo ya Wizara, Taasisi, Balozi, na
huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo Viwanja vya michezo, Hosipitali,
maeneo ya kupumzikia, Maeneo ya Biashara .
Aliongeza kuwa upatikanaji wa
huduma katika Mji wa Serikali utakuwa wa uhakika na utakuwa
umerahisishwa kutokana na kuwepo kwa Taasisi za Serikali na Wizara zote
katika eneo moja.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu
wa Shirika la Nyumba la Taifa Bw. Nehemia Mchechu amesema kuwa ni muhimu
kuvutia wawekezaji kuja kuwekeza mkoani Dodoma kutokana na mipango ya
Serikali kujenga mji huo wa Kisasa wa Serikali.
Aliongeza kuwa mawazo ya awali ya
namna ya kujenga mji huo wa Kisasa wa Serikali yapo na kinachosubiriwa
ni hatua mbalimbali za kiutendaji zitakazowezesha kutekelezwa kwa mradi
huo.
Uamuzi wa Serikali kuhamia Dodoma
umepata msukumo katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Tano
inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli na tayari utekelezaji wake
unaendelea ambapo Mawaziri wote wameshahamia Dodoma, Makatibu Wakuu na
Watumishi Wengine wa Serikali pia wameshahamia.
No comments:
Post a Comment