Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiwa pamoja na Mgombea nafasi ya Udiwani Kata ya Nata, Bwana John Cheyo Mabonde wakifanya matembezi wakati wa kuelekea kwenye viwanja vya kampeni katika tawi la Mwamalulu katika Kijiji cha Mwamalulu Kata hiyo ya Nata, Katika jimbo la Nzega Vijijini, jana jioni Novemba 24,2017.
Andrew Chale
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM-Bara), Rodrick Mpogolo, Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla leo Novemba 25,2017, wanatarajia kumnadi mgombea nafasi ya Udiwani katika uchaguzi mdogo wa marudio Bwana John Cheyo Mabonde anayewania kiti cha Udiwani Kata ya Nata iliyopo Nzega Vijijini.
Kampeni hizo za kishindo zinatarajia kufikia tamati leo hii katika Kata hiyo ya Nata ambapo tayari Mgombea huyo ameweza kuninadi katika maeneo mbalimbali ya Kata hiyo.
Awali Dk.Kigwangalla ambaye ni Mbunge wa jimbo hilo, aliwataka wananchi kuhakikisha wanaendelea kulinda Kata yao ambayo walishashinda tokea 2015.
“Ushindi tulishamaliza. Tulishinda Kata hii 2015. Kura za kesho ni kuhitimisha tu ushindi wetu hivyo tujitokeze kwa wingi kupiga kura za ndio kwa CCM kwa kumchagua Mabonde.” Alieleza Dk.Kigwangalla wakati wa kumandi mgombea huyo katika kampeni zilizofanyika jana Novemba 24 kwenye tawi la Mwamalulu.
Kwa upande wake, Mgombea udiwani huyo Bwana Mabonde aliendelea kuwashukuru wananchi wa Kata hiyo kwa kuendelea kujitokeza kwa wingi kwenye kampeni zake huku akiwataka kuhakikisha wanaendelea kujitokeza katika kupiga kura siku ya Novemba 26 katika kupiga kura za ndio.
“Kura zenu ni mtaji wetu. Nawaombeni sana ndugu zangu, wana Nata kujitokeza kwa wingi kupiga kura. Ushindi huu ni wetu ili kuendelea kumuunga mkono Rais John Pombe Magufuli katika vita yake ya kiuchumi na kupambanana mafisadi.
Aidha, katika mkutano huo wa jana jioni, ambao pia ulikuwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho waliweza kuwashukuru wananchi kwa kuendelea kukiunga mkono Chama cha Mapinduzi (CCM).
No comments:
Post a Comment