Thursday, November 9, 2017

BREAKING NEWS: WAZIRI WA KILIMO DKT TIZEBA AMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI MKUU WA BODI YA SUKARI TANZANIA

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania Ndg Henry J. Semwanza

Na Mathias Canal, Dodoma

Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba amemuagiza Katibu mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe  kumsimamisha kazi mara moja Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania Ndg Henry J. Semwanza kuanzia leo Novemba 9, 2017.

Kwa agizo hilo lililotolewa na Waziri wa Kilimo Dkt Tizeba, Mkurugenzi huyo atatakiwa kurejea kwa mwajiri wake ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo kwa ajili ya kupangiwa kazi nyingine.

Simwanza anasimamishwa kazi kutokana na mwenendo wake wa utendaji akiwa Msimamizi Mkuu wa Bodi ya Sukari kutoridhisha.

Simwanza amehudumu katika nafasi hiyo akiwa Mkurugenzi wa Bodi ya Sukari tangu mwaka 2011.

MWISHO

No comments:

Post a Comment