shughuli zao kwa urahisi zaidi hasa wanapokuwa wakihama hama kutafuta malisho ya mifugo.“ Katika kuwasajili wananchi moja ya kikwazo kikubwa hapa ni elimu ya kujua kusoma na kuandika na lugha. Lakini kama Serikali tumejipanga kwa kushirikiana na Mamlaka ya Vitambulisho katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma hii kwa kutumia wataalamu tulionao” alisisitiza.Wananchi katika Wilaya hiyo ambao asilimia kubwa ni wa jamii ya Maasai; wameeleza kufurahishwa na hatua ya Serikali kutoa Vitambulisho vya Taifa kwani kwa muda mrefu wamekuwa wakipata bughudha kubwa toka upande wa Kenya wanapokuwa malishoni kwakuwa wananchi wa Kenya tayari wanatumia Vitambulisho kuwatambua maarufu kama “Kipande”.Wilaya ya Longido inakisiwa kuwa na takribani wananchi 120,000 ambao watasajiliwa Vitambulisho vya Taifa, huku idadi ya wananchi wasiojua kusoma na kuandika ikikadiwa kuwa zaidi ya asilimia 65%.
Saturday, October 28, 2017
VITAMBULISHO VYA TAIFA KUWANUFAISHA WAFUGAJI WILAYA YA LONGIDO
Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe. Godfrey Daniel Chongolo leo
amekagua maendeleo ya zoezi la Usajili na Utambuzi wa Watu lenye
kulenga kutoa Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa Wilaya hiyo.Katika
ziara hiyo Mhe. Chongolo amesema kwakuwa idadi kubwa ya wananchi wa
Wilaya hiyo ni kutoka jamii ya Wafugaji; Kama Wilaya wamejipanga katika
kuhakikisha wananchi wote wenye sifa wanasajiliwa na kupata Vitambulisho
vya Taifa vitakavyosaidia kuondokana na changamoto kubwa ya Wahamiaji
Haramu; changamoto ambayo ni kubwa kutokana na kupakana na nchi nyingi
jirani. Faida nyingine ni kuwawezesha wananchi wake ambao niwa jamii ya
wafugaji kufanya
shughuli zao kwa urahisi zaidi hasa wanapokuwa wakihama hama kutafuta malisho ya mifugo.“ Katika kuwasajili wananchi moja ya kikwazo kikubwa hapa ni elimu ya kujua kusoma na kuandika na lugha. Lakini kama Serikali tumejipanga kwa kushirikiana na Mamlaka ya Vitambulisho katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma hii kwa kutumia wataalamu tulionao” alisisitiza.Wananchi katika Wilaya hiyo ambao asilimia kubwa ni wa jamii ya Maasai; wameeleza kufurahishwa na hatua ya Serikali kutoa Vitambulisho vya Taifa kwani kwa muda mrefu wamekuwa wakipata bughudha kubwa toka upande wa Kenya wanapokuwa malishoni kwakuwa wananchi wa Kenya tayari wanatumia Vitambulisho kuwatambua maarufu kama “Kipande”.Wilaya ya Longido inakisiwa kuwa na takribani wananchi 120,000 ambao watasajiliwa Vitambulisho vya Taifa, huku idadi ya wananchi wasiojua kusoma na kuandika ikikadiwa kuwa zaidi ya asilimia 65%.
Baadhi
ya wananchi wa Wilaya ya Longido wakipigwa picha na mashine maalumu ya
Usajili wakati zoezi hilo likiendelea Wilayani hapo.
Hawa ni watendaji wa Vijiji vya Namanga na Longido wakichambua fomu za wananchi wao ili kutoa fursa ya kusajiliwa.
Mhe.
Godfrey Daniel Chongolo (Mwenye suti- kushoto) akikagua fomu za
wananchi ambao wamesajiliwa kwa ajili ya kupigwa Picha na Saini ya
Kielektroniki alipotembelea vituo vya Usajili Kata za Namanga na Karatu.
Katikati ni Afisa Usajili Wilaya ya Longido Bw. Emmanuel Tarimo na
Kulia ni Bw. Elisha Noel Afisa Usajili Msaidizi.
Mhe.
Chongolo akiangalia namna taarifa za mwananchi zinavyoingizwa kwenye
mfumo kwa kutumia mashine maalumu (Mobile Enrollment Unit –MEU).
Michuzi
shughuli zao kwa urahisi zaidi hasa wanapokuwa wakihama hama kutafuta malisho ya mifugo.“ Katika kuwasajili wananchi moja ya kikwazo kikubwa hapa ni elimu ya kujua kusoma na kuandika na lugha. Lakini kama Serikali tumejipanga kwa kushirikiana na Mamlaka ya Vitambulisho katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma hii kwa kutumia wataalamu tulionao” alisisitiza.Wananchi katika Wilaya hiyo ambao asilimia kubwa ni wa jamii ya Maasai; wameeleza kufurahishwa na hatua ya Serikali kutoa Vitambulisho vya Taifa kwani kwa muda mrefu wamekuwa wakipata bughudha kubwa toka upande wa Kenya wanapokuwa malishoni kwakuwa wananchi wa Kenya tayari wanatumia Vitambulisho kuwatambua maarufu kama “Kipande”.Wilaya ya Longido inakisiwa kuwa na takribani wananchi 120,000 ambao watasajiliwa Vitambulisho vya Taifa, huku idadi ya wananchi wasiojua kusoma na kuandika ikikadiwa kuwa zaidi ya asilimia 65%.
No comments:
Post a Comment