Naibu waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa (Mb) akikagua maghala ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula (NFRA) Mara baada ya kutembelea Ofisi hizo Mtaa wa Njiro Mkoani Arusha. Picha Zote Na Mathias Canal.
Naibu waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa (Mb) akikagua maghala ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula (NFRA) Mara baada ya kutembelea Ofisi hizo Mtaa wa Njiro Mkoani Arusha. Leo Octoba 29, 2017Naibu waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza jambo wakati wa kikao cha kazi na uongozi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula (NFRA). Leo Octoba 29, 2017
Meneja wa Kanda ya Arusha Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula (NFRA) Ndg Ramadhan A. Nondo akitoa taarifa fupi kuhusu ukusanyaji wa mazao mbele ya Naibu waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa kikao cha pomoja. Leo Octoba 29, 2017
Muonekano wa Maghala ya wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula (NFRA) yakiwa katika hali nzuri
Meneja wa Kanda ya Arusha Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula (NFRA) Ndg Ramadhan A. Nondo akitoa taarifa fupi kuhusu ukusanyaji wa mazao mbele ya Naibu waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa kikao cha pomoja. Leo Octoba 29, 2017
Na Mathias Canal, Arusha
Naibu waziri wa Kilimo Mhe Mary
Mwanjelwa leo Octoba 29, 2017 ametembelea Ofisi za Wakala wa Taifa wa Hifadhi
ya chakula zilizopo Mtaa wa Njiro Mkoani Arusha ili kujionea namna wanavyofanya
kazi kutekeleza majukumu yao.
Mhe Mwanjelwa ametembelea Ofisi hizo
ambapo pamoja na mambo mengine amekagua maghala yanayotumika kuhifadhi chakula
ambapo amejionea ukubwa wa maghala hayo na jinsi kanda ya Arusha ilivyo na
uwezo wa kuhifadhi chakula wastani wa Tani 39000.
Pia alijionea akiba kubwa iliyopo
ghalani ya mahindi katika msimu huu wa mwaka 2017/2018 ambayo ni Jumla ya
tani 3,997.664 ambazo hizo ni pamoja na salio la mahindi la msimu uliopita
2016/2017 ambazo zilikuwa Tani 2,997.664
Akizungumza na baadhi ya wafanyakazi
wa NFRA Mhe Mwanjelwa aliwapongeza kwa uwajibikaji huku akiwasihi kuongeza
ufanisi na ubunifu katika kutekeleza majukumu yao ikiwa ni pamoja na kuzikabili
changamoto mbalimbali ikiwemo ile ya ufinyu wa bajeti.
Mhe Mwanjelwa alisema kuwa sifa ya
mtumishi mzuri ni yule mwenye uwezo wa kukabiliana na changamoto ili kutimiza
adhma ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika kukuza ufanisi katika kazi
kwa kutimiza vyema wajibu kwa kuwa wabunifu.
Alisema kuwa watumishi wanapaswa
kuongeza ushirikiano na Ari mpya ya kazi kwa kufanya kazi kwa weledi kuachana
na kufanya kazi kwa mazoea.
Chimbuko la Wakala wa Taifa wa
Hifadhi ya chakula lilitokana na lililokuwa shirika la Usagishaji la Taifa
(NMC) mwaka 1990 ambapo dhumuni kubwa ilikuwa ni kuwepo na kitengo maalumu cha
kununua, kuhifadhi, kuhudumia chakula Sehemu zenye upungufu wa chakula na
kulinda bei ya soko la mahindi kwa mlaji mbali na shughuli zilizokuwa
zikifanywa na NMC.
Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya
chakula ipo chini ya Wizara ya kilimo na Msimamizi Mkuu wa shughuli zote za
Wakala ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala (CEO).
MWISHO.
No comments:
Post a Comment