Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na kiongozi na mbashiri mkuu wa Jumuiya ya waislamu wa
Ahmadiya Tanzania,Tahir Mahmood, kabla ya kufungua mkutano mkuu wa 48 wa
jumuiya hiyo Mbande, Temeke, Jijini Dar es salaam Oktoba 1, 2017.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza na waumini wa Jumuiya ya waislamu wa Ahmadiya Tanzania,
kabla ya kufungua mkutano mkuu wa 48 wa Jumuiya hiyo huko Mbande,
Temeke, Jijini Dar es salaam Oktoba 1, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza na waumini wa Jumuiya ya waislamu wa Ahmadiya Tanzania,
kabla ya kufungua mkutano mkuu wa 48 wa Jumuiya hiyo huko Mbande,
Temeke, Jijini Dar es salaam Oktoba 1, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akipokea kitabu kutoka kwa Katibu wa Malezi Jumuiya ya waislamu wa
Ahmadiya Tanzania, Mahmood Hamsin, baada ya kufungua mkutano mkuu wa 48
wa jumuiya hiyo Mbande, Temeke, Jijini Dar es salaam Oktoba 1, 2017.
(kulia) ni. kiongozi na mbashiri mkuu wa Jumuiya ya waislamu wa Ahmadiya
Tanzania,Tahir Mahmood. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amewaomba Viongozi wa Jumuiya na Taasisi zote za kidini nchini
wahakikishe wanawapiga vita watu wote wanaopanga na kutaka kuvuruga
amani na utulivu uliopo nchini kwa sababu watakwamisha maenendeleo.
Amesema Serikali inaelewa kwamba
dini ni miongoni mwa vyanzo muhimu vya maendeleo ya ustaarabu wa
mwanadamu kwani inatoa elimu ya maadili mema yenye kuwafanya waumini
waepukane na maovu mbalimbali.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo
(Jumapili Oktoka 01, 2017) wakati akifungua mkutano Mkuu wa mwaka wa 48
wa Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya uliofanyika katika eneo la Kitonga
kata ya Msongola wilayani Ilala, Dar es Salaam.
Amesema kila Mtanzania anatakiwa
ahakikishe anadhibiti matukio yote yenye viashiria vya uvunjifu wa amani
kwa kutoa taarifa katika mamlaka husika.”Tanzania ni nchi salama na
yenye utulivu, hivyo ni lazima wote tushirikiane kuitunza.”
“Napenda niwahakikishieni kuwa
Serikali inaunga mkono juhudi za Jumuiya za kidini katika kupiga vita
maovu ya kila aina; mathalan utumiaji wa dawa za kulevya, wizi, rushwa,
uzinzi ambao husababisha madhara mengi ukiwemo ugonjwa wa UKIMWI.”
Amesema iwapo dini zetu
zitatumika vizuri tutaweza kwa haraka sana kutekeleza agizo la Rais Dkt.
John Magufuli la ‘Hapa kazi tu’ kwani kila mtu ataepuka uzembe na
kuwajibika ipasavyo.
Waziri Mkuu amesema ana imani
kwamba jumuiya hiyo kama zilivyo taasisi zingine za kidini itaendeleza
kazi kubwa ya kupambana na maovu katika jamii yetu kwa kuwapatia waumini
wao na wananchi kwa ujumla elimu na maarifa ya kuboresha tabia zao na
maadili yao kiroho.
Amesema amani na utulivu uliopo
nchini unatokana na mambo mengi ikiwemo na wananchi kupata ustawi,
kuweza kufanya shughuli zao vizuri na kuwa na imani na Serikali yao,
ambayo imejiwekea mikakati ya kuhakikisha wananchi hususan wanyonge
wanapata faraja ndani ya nchi yao.
Waziri Mkuu amesema mambo
yameweza kupatikana baada ya Serikali kupambana na rushwa na ufisadi
pamoja na kuimarisha maadili ya watumishi wa umma, ambayo vimekuwa ni
vyanzo vya kupotea kwa amani na utulivu katika baadhi ya nchi.
“Serikali imeweka mikakati
madhubuti ya kupambana na ufisadi, kupitia mikataba mibovu na kuimarisha
maadili ili kujenga imani kwa wananchi, kuondoa migongano na tofauti ya
kipato, kuwa na matumizi mazuri ya rasilimali za umma, kuleta tija kwa
kuongeza thamani ya huduma na kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato.”
Awali, Amir na Mbashiri Mkuu wa
Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya Tanzania, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry
amesema Jumuiya hiyo imekuwa ikifanya mikutano kila mwaka kwa lengo la
kukumbushana misingi sahihi ya dini tukufu ya kiislam pamoja na kukuza
undugu wao.
Sheikh Chaudhry amesema mkutano
wa mwaka huu umejumisha watu zaidi ya 4,000 kutoka mikoa yote ya
Tanzania Bara na Visiwani pamoja na wageni kutoka nchi za Uingereza,
Canada, Rwanda, Uganda, Ujerumani, Kenya, Burundi, Malawi na Jamuhuri ya
Kidemokrasi ya Congo (DRC).
Amesema Jumuiya hiyo mbali na
masuala ya kidini pia inatoa huduma mbalimbali za kijamii kama elimu,
maji na afya kwenye mikoa tofauti tofauti nchini.
No comments:
Post a Comment