Shirikisho la ngumi Tanzania
(BFT) limeanda mashindano ya ngumi yaliyofanyika tarehe 30/09/2017 kati
ya timu yaTaifa ya Ngumi dhidi ya timu ya Ngome inayomilikiwa na Jeshi
la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) Mashindano hayo yalikuwa ni jaribio la
kwanza kwa timu yetu ya ngumi inayoendelea na mazoezo kwa ajili ya
maandalizi ya kushiriki Mashindano ya Jumuiya ya Madola yatakayofanyika
Gold Coast, AUSTRALIA Aprili 2018. Na yalikuwa pia na lengo la uzinduzi
rasmi wa mazoezi ya kujiandaa na mashindano hayo.
Mashindano hayo ya siku moja yalifunguliwa na Mkurugenzi wa michezo Tanzania ndugu Yusuph Singo.
Timu hiyo ya Taifa iliyo na
mabondia wa kiume na kike imeanza vema jaribio hilo la kwanza baada ya
kushinda michezo tisa dhidi ya mitatu walioshinda Ngome kwa upande wa
wanaume baada ya kuwa mazoezini tangu mwanzoni mwa mwezi wa nane 2018.
Kwa upande wa mabondia wa kike wote walioshiriki ni kutoka timu ya Taifa.
Matokeo yalikuwa kama ifuatavyo:-
WANAUME,
- Herman Shekivuli (Taifa) alimshinda Issa Kpaya (Ngome) 49 Kgs.
- Geoge Costantino (Taifa) alimshinda John Christian (Ngome) 52 Kgs
- Ezra Paul (Taifa) alimshinda Emmanuel Marwa ( Ngome) 56 Kgs
- Ismail Galiatana (Taifa) alimshinda Fabian Gaudence (Ngome) 60 Kgs
- Mohameda Juma (Taifa) alimshinda Isiaka Lusajo (Taifa) 64 Kgs
- Kassim Butike (Taifa) alimshinda Julius Nickson (Ngome) 69 Kgs
- Selemani Kidunda (Taifa) alimshinda Daudi Kuzenza (Ngome) 75 Kgs
- Yusuph Changarawe (Taifa) alimshinda Twalibu Kinyogori (Ngome) 81 Kgs
- Haruna Swanga (Taifa) alimshinda Alex Sitta (Taifa)
- Alex Michael Ngome) alimshinda Mwalimu Ngayana (Taifa)
- Kelvin Kapinga (Ngome) alimshinda Said Ramadhani ( Taifa)
- Batele Abed (Ngome ) alimshinda Mwinyi Ally (Huru)
WANAWAKE
- Siwatu Kimbe (Taifa) alimshinda Lusiana Gadani (Taifa)
- Safina Fussi (Taifa) alimshinda Asha Juma (Taifa)
- Najma Isike (Taifa) alimshinda Monica Malango (Taifa)
- Mariam Macho (Taifa) alimshinda Naomi Shoo Taifa)
- Grace Mwakamale (Taifa) alimshinda Leonia Kalimunju ( Taifa)
Aidha wakati wa kufungua
mashindano hayo Mkurugenzi wa michezo Yusuph Singo alisema serikali
imeona na inatambua jitihada zinazofanywa na BFT katika kuendeleza
mchezo wa Ngumi Tanzania na hasa hatua za kuandaa timu ya Taifa mapema
kwa ajili ya kushiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola 2018.
Alisema serikali itakuwa karibu na BFT kuhakikisha mazoezi hayo yanaendelea vizuri na kusaidiana kuondoa changamoto zilizopo.
Alieleza kuwa kwa hivi sasa
serikali ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha mpango wa timu ya
Taifa ya ngumi kwenda nchini Cuba kwa ajili ya mazoezi ya kushiriki
mashindano ya Jumuya ya madola 2018.
Mwisho BFT imeahidi kuwa
mashindano hayo yatakuwa yanafanyika kila wa kila mwezi kwa kushindana
na timu za ndani na nje ya Tanzania.
Taarifa hizi zinaletwa kwena na
Makore Mashaga.
KATIBU MKUU (BFT)
No comments:
Post a Comment