WANAMUZIKI wanaounda kundi linalotikisa Bongo kwa sasa la Rostam, Roma
Mkatoliki na Stamina, wamefunguka kuwa, endapo mmoja kati yao akibaini
mwenzake amechepuka, basi ndiyo itakuwa mwisho wa uhai wa kundi hilo.
Wawili hao kwa sasa wanatamba na wimbo wao wa Huku Ama Kule ambao
unafanya vizuri kwenye vituo vya redio na runinga.
Roma amesema: “Yaani sisi kila mtu hapa alipo anamlinda mwenzake
kuhakikisha hapigi, hachepuki licha ya kwamba kuna vishawishi vingi
ambavyo tunakutana navyo wakati tukisaka ugali wetu wa kila siku.
“Kama ikitokea siku m i m i nimemfuma Stamina au yeye akanifumania nipo
na mwanamke mwingine tofauti na mke wangu tukifanya mambo ya kimapenzi,
basi hapo ndiyo utakuwa mwisho wa kundi hili.”
No comments:
Post a Comment